063 - Al-Munaafiquwn

 

  الْمُنَافِقُون

 

063-Al-Munaafiquwn

 

 

063-Al-Munaafiquwn: Utangulizi Wa Suwrah

 

Alhidaaya.com 

 

 

 

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

 

 

إِذَا جَاءَكَ الْمُنَافِقُونَ قَالُوا نَشْهَدُ إِنَّكَ لَرَسُولُ اللَّـهِ ۗ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ إِنَّكَ لَرَسُولُهُ وَاللَّـهُ يَشْهَدُ إِنَّ الْمُنَافِقِينَ لَكَاذِبُونَ﴿١﴾

1. Wanapokujia wanafiki husema: Tunashuhudia kwamba wewe bila shaka ni Rasuli wa Allaah. Na Allaah Anajua kuwa wewe ni Rasuli Wake, na Allaah Anashuhudia kuwa hakika wanafiki ni waongo.[1]

 

 

 

 

اتَّخَذُوا أَيْمَانَهُمْ جُنَّةً فَصَدُّوا عَن سَبِيلِ اللَّـهِ ۚ إِنَّهُمْ سَاءَ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ﴿٢﴾

2. Wamefanya viapo vyao kuwa ni ngao, hivyo wakazuia Njia ya Allaah. Hakika ni maovu mno waliyokuwa wakiyatenda.

 

 

 

 

ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ آمَنُوا ثُمَّ كَفَرُوا فَطُبِعَ عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ فَهُمْ لَا يَفْقَهُونَ﴿٣﴾

3. Hiyo ni kwa sababu ya kuwa waliamini, kisha wakakufuru, basi ukapigwa mhuri juu ya nyoyo zao, kwa hiyo hawafahamu lolote.

 

 

 

 

وَإِذَا رَأَيْتَهُمْ تُعْجِبُكَ أَجْسَامُهُمْ ۖ وَإِن يَقُولُوا تَسْمَعْ لِقَوْلِهِمْ ۖ كَأَنَّهُمْ خُشُبٌ مُّسَنَّدَةٌ ۖ يَحْسَبُونَ كُلَّ صَيْحَةٍ عَلَيْهِمْ ۚ هُمُ الْعَدُوُّ فَاحْذَرْهُمْ ۚ قَاتَلَهُمُ اللَّـهُ ۖ أَنَّىٰ يُؤْفَكُونَ﴿٤﴾

4. Na unapowaona, inakupendezesha miili yao, na wanaposema, unasikiliza kauli zao. Lakini wao ni kama magogo yaliyoegemezwa. Wanadhania kuwa kila ukelele unaopigwa ni kwa ajili yao. Hao ndio maadui, basi tahadhari nao, Allaah Awaangamizilie mbali. Namna namna gani wanavyoghilibiwa!

 

 

 

 

وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ تَعَالَوْا يَسْتَغْفِرْ لَكُمْ رَسُولُ اللَّـهِ لَوَّوْا رُءُوسَهُمْ وَرَأَيْتَهُمْ يَصُدُّونَ وَهُم مُّسْتَكْبِرُونَ﴿٥﴾

5. Wanapoambiwa: Njooni ili Rasuli wa Allaah akuombeeni maghfirah, hupindisha vichwa vyao, na utawaona wanakwepa na huku wao ni wenye kutakabari.

 

 

 

 

سَوَاءٌ عَلَيْهِمْ أَسْتَغْفَرْتَ لَهُمْ أَمْ لَمْ تَسْتَغْفِرْ لَهُمْ لَن يَغْفِرَ اللَّـهُ لَهُمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْفَاسِقِينَ﴿٦﴾

6. Ni sawasawa juu yao, ukiwaombea maghfirah au usiwaombee, Allaah Hatowaghufuria kamwe. Hakika Allaah Haongoi watu mafasiki.

 

 

 

 

هُمُ الَّذِينَ يَقُولُونَ لَا تُنفِقُوا عَلَىٰ مَنْ عِندَ رَسُولِ اللَّـهِ حَتَّىٰ يَنفَضُّوا ۗ وَلِلَّـهِ خَزَائِنُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَلَـٰكِنَّ الْمُنَافِقِينَ لَا يَفْقَهُونَ﴿٧﴾

7. Wao ndio wale wasemao: Msitoe mali kwa ajili ya walioko kwa Rasuli wa Allaah mpaka waondokelee mbali.  Na ilhali ni za Allaah Pekee hazina za mbingu na ardhi, lakini wanafiki hawafahamu.

 

 

 

 

 

يَقُولُونَ لَئِن رَّجَعْنَا إِلَى الْمَدِينَةِ لَيُخْرِجَنَّ الْأَعَزُّ مِنْهَا الْأَذَلَّ ۚ وَلِلَّـهِ الْعِزَّةُ وَلِرَسُولِهِ وَلِلْمُؤْمِنِينَ وَلَـٰكِنَّ الْمُنَافِقِينَ لَا يَعْلَمُونَ﴿٨﴾

8. Wanasema: Tutakaporudi Madiynah, mwenye hadhi zaidi lazima atamfukuza humo aliye dhalili. Na ilhali utukufu ni wa Allaah na wa Rasuli Wake na wa Waumini, lakini wanafiki hawajui.

 

 

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تُلْهِكُمْ أَمْوَالُكُمْ وَلَا أَوْلَادُكُمْ عَن ذِكْرِ اللَّـهِ ۚ وَمَن يَفْعَلْ ذَٰلِكَ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْخَاسِرُونَ﴿٩﴾

9. Enyi walioamini! Zisikupurukusheni mali zenu wala watoto wenu mkaacha kumdhukuru Allaah. Na yeyote atakayefanya hivyo, basi hao ndio waliokhasirika.[2]

 

 

 

 

وَأَنفِقُوا مِن مَّا رَزَقْنَاكُم مِّن قَبْلِ أَن يَأْتِيَ أَحَدَكُمُ الْمَوْتُ فَيَقُولَ رَبِّ لَوْلَا أَخَّرْتَنِي إِلَىٰ أَجَلٍ قَرِيبٍ فَأَصَّدَّقَ وَأَكُن مِّنَ الصَّالِحِينَ﴿١٠﴾

10. Na toeni katika yale Tuliyokuruzukuni kabla hayajamfikia mmoja wenu mauti akasema: Rabb wangu! Lau Ungeliniakhirisha mpaka muda wa karibu hivi, nikatoa swadaqah na nikawa miongoni mwa Swalihina.[3]

 

 

 

وَلَن يُؤَخِّرَ اللَّـهُ نَفْسًا إِذَا جَاءَ أَجَلُهَا ۚ وَاللَّـهُ خَبِيرٌ بِمَا تَعْمَلُونَ﴿١١﴾

11. Lakini Allaah Haiakhirishi kamwe nafsi yeyote inapokuja ajali yake, na Allaah Ni Mjuzi wa Khabari za dhahiri na siri kwa yale myatendayo.

 

 

 

[1] Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:

 

Kuanzia Aayah hii ya kwanza hadi namba (8) kuna kisa cha mnafiki mkuu ‘Abdullaah bin Saluwl alivyotaka kumdhalilisha Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) na Waumini na kutaka kuwafukuza katika mji wa Madiynah.  Bonyeza kiungo kifuatacho:  

 

063-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Munaafiquwn Aayah 1-8: إِذَا جَاءَكَ الْمُنَافِقُونَ قَالُوا نَشْهَدُ إِنَّكَ لَرَسُولُ اللَّـهِ

 

[2] Maonyo Ya Kughafilika Kumdhukuru Allaah:

 

Rejea Twaahaa (20:124) kwenye maonyo ya kughafilika na kumdhukuru Allaah. Na rejea Al-Ahzaab (33:41) kwenye fadhila za kumdhukuru Allaah.

 

[3] Binaadam Hujuta Anapotolewa Roho Akiwa Ni Kafiri Au Muasi Au Asipotenda Mema:

 

Allaah (سبحانه وتعالى) Ameonya majuto ya watu kutokumtii na kutamani kurudi duniani kutenda mema. Miongoni mwa Kauli Zake ni ifuatayo:

 

حَتَّىٰ إِذَا جَاءَ أَحَدَهُمُ الْمَوْتُ قَالَ رَبِّ ارْجِعُونِ ﴿٩٩﴾ لَعَلِّي أَعْمَلُ صَالِحًا فِيمَا تَرَكْتُ ۚ كَلَّا ۚ إِنَّهَا كَلِمَةٌ هُوَ قَائِلُهَا ۖ وَمِن وَرَائِهِم بَرْزَخٌ إِلَىٰ يَوْمِ يُبْعَثُونَ ﴿١٠٠﴾

Mpaka yatakapomfikia mmoja wao mauti, atasema: Rabb wangu! Nirejesheni (duniani). Ili nikatende mema katika yale niliyoyaacha. (Ataambiwa) Laa hasha! Hakika hilo ni neno alisemalo yeye tu.  Na mbele yao kuna Barzakh[3] mpaka Siku watakayofufuliwa. [Al-Muuminuwn (23:99-100)]

 

Rejea pia Al-A’raaf (7:53), Ibraahiym (14:44), As-Sajdah (32:12), Al-An'aam (6:27-28), Ash-Shuwraa (42:44), Faatwir (35:37), Ghaafir (40:11-12), Az-Zumar (39:53-58).

 

 

Share