074 - Al-Muddath-thir

 

   الْمُدَّثِّر

 

074-Al-Muddath-thir

 

074-Al-Muddath-thir: Utangulizi Wa Suwrah

 

Alhidaaya.com

 

 

 

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

 

 

يَا أَيُّهَا الْمُدَّثِّرُ﴿١﴾

1. Ee mwenye kujigubika![1]

 

 

 

قُمْ فَأَنذِرْ﴿٢﴾

2. Simama uonye.

 

 

 

وَرَبَّكَ فَكَبِّرْ﴿٣﴾

3. Na Rabb wako mtukuze. 

 

 

 

وَثِيَابَكَ فَطَهِّرْ﴿٤﴾

4. Na nguo zako toharisha.[2]

 

 

 

وَالرُّجْزَ فَاهْجُرْ﴿٥﴾

5. Na masanamu na machafu endelea kuepukana nayo.

 

 

 

 

وَلَا تَمْنُن تَسْتَكْثِرُ﴿٦﴾

6. Na wala usifanye fadhila kwa ajili ya kutaraji kukithirishiwa.

 

 

 

وَلِرَبِّكَ فَاصْبِرْ﴿٧﴾

7. Na kwa ajili ya Rabb wako subiri.

 

 

 

فَإِذَا نُقِرَ فِي النَّاقُورِ﴿٨﴾

8. Litakapopulizwa baragumu kwa sauti kali.

 

 

 

فَذَٰلِكَ يَوْمَئِذٍ يَوْمٌ عَسِيرٌ﴿٩﴾

9. Basi hiyo itakuwa ni Siku ngumu mno.[3]

 

 

 

عَلَى الْكَافِرِينَ غَيْرُ يَسِيرٍ﴿١٠﴾

10. Kwa makafiri si nyepesi.

 

 

 

ذَرْنِي وَمَنْ خَلَقْتُ وَحِيدًا﴿١١﴾

11. Niache Mimi na yule Niliyemuumba Pekee.[4]

 

 

 

وَجَعَلْتُ لَهُ مَالًا مَّمْدُودًا﴿١٢﴾

12. Na Nikamjaalia mali tele.

 

 

 

وَبَنِينَ شُهُودًا﴿١٣﴾

13. Na watoto walio naye nyakati zote.

 

 

 

وَمَهَّدتُّ لَهُ تَمْهِيدًا﴿١٤﴾

14. Na Nikamkunjulia njia zote za maisha mazuri.

 

 

 

ثُمَّ يَطْمَعُ أَنْ أَزِيدَ﴿١٥﴾

15. Kisha anatumaini Nimuongezee.

 

 

 

كَلَّا ۖ إِنَّهُ كَانَ لِآيَاتِنَا عَنِيدًا﴿١٦﴾

16. Laa, hasha!  Hakika yeye amekuwa anidi na mpinzani wa Aayaat (na Ishara, Dalili, Hoja) Zetu.

 

 

 

سَأُرْهِقُهُ صَعُودًا﴿١٧﴾

17. Nitamshurutisha adhabu ngumu asiyoiweza.

 

 

إِنَّهُ فَكَّرَ وَقَدَّرَ﴿١٨﴾

18. Hakika yeye alitafakari na akakadiria.[5]   

 

 

فَقُتِلَ كَيْفَ قَدَّرَ﴿١٩﴾

19. Basi alaaniwe na aangamie mbali. Namna gani kakadiria?!  

 

 

 

ثُمَّ قُتِلَ كَيْفَ قَدَّرَ﴿٢٠﴾

20. Kisha alaaniwe na aangamie mbali. Namna gani kakadiria?!

 

 

 

ثُمَّ نَظَرَ﴿٢١﴾

21. Kisha akatazama.

 

 

 

ثُمَّ عَبَسَ وَبَسَرَ﴿٢٢﴾

22. Kisha akakunja kipaji na akafinya uso kwa ghadhabu.

 

 

 

ثُمَّ أَدْبَرَ وَاسْتَكْبَرَ﴿٢٣﴾

23. Kisha akageuka nyuma na akatakabari.

 

 

 

فَقَالَ إِنْ هَـٰذَا إِلَّا سِحْرٌ يُؤْثَرُ﴿٢٤﴾

24. Akasema: Hii (Qur-aan) si chochote isipokuwa ni sihiri inayonukuliwa. 

 

 

 

 

إِنْ هَـٰذَا إِلَّا قَوْلُ الْبَشَرِ﴿٢٥﴾

25. Hii si chochote isipokuwa ni maneno ya binaadam tu.

 

 

 

سَأُصْلِيهِ سَقَرَ﴿٢٦﴾

26. Nitamuingiza Saqar[6] aungue.

 

 

 

 

وَمَا أَدْرَاكَ مَا سَقَرُ﴿٢٧﴾

27. Na kipi kitakachokujulisha ni nini hiyo Saqar?

 

 

 

لَا تُبْقِي وَلَا تَذَرُ﴿٢٨﴾

28. (Ni moto ambao) haubakishi wala hauachi (kitu kisiunguzwe).

 

 

 

لَوَّاحَةٌ لِّلْبَشَرِ﴿٢٩﴾

29. Wenye kubabua vibaya ngozi.

 

 

 

عَلَيْهَا تِسْعَةَ عَشَرَ﴿٣٠﴾

30. Juu yake wako (walinzi) kumi na tisa.

 

 

 

 

وَمَا جَعَلْنَا أَصْحَابَ النَّارِ إِلَّا مَلَائِكَةً ۙ وَمَا جَعَلْنَا عِدَّتَهُمْ إِلَّا فِتْنَةً لِّلَّذِينَ كَفَرُوا لِيَسْتَيْقِنَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ وَيَزْدَادَ الَّذِينَ آمَنُوا إِيمَانًا ۙ وَلَا يَرْتَابَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ وَالْمُؤْمِنُونَ ۙ وَلِيَقُولَ الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٌ وَالْكَافِرُونَ مَاذَا أَرَادَ اللَّـهُ بِهَـٰذَا مَثَلًا ۚ كَذَٰلِكَ يُضِلُّ اللَّـهُ مَن يَشَاءُ وَيَهْدِي مَن يَشَاءُ ۚ وَمَا يَعْلَمُ جُنُودَ رَبِّكَ إِلَّا هُوَ ۚ وَمَا هِيَ إِلَّا ذِكْرَىٰ لِلْبَشَرِ﴿٣١﴾

31. Na Hatukuweka walinzi wa moto isipokuwa ni Malaika. Na Hatukufanya idadi yao isipokuwa iwe ni jaribio kwa wale waliokufuru, ili wayakinishe wale waliopewa Kitabu, na iwazidishie iymaan wale walioamini, na wala wasitie shaka wale waliopewa Kitabu na Waumini. Na ili wale waliokuwa na maradhi nyoyoni mwao[7] (ya unafiki, shaka) na makafiri waseme: Allaah Amekusudia nini kwa mfano huu? Hivyo ndivyo Allaah Anavyompotoa Amtakaye na Anamhidi Amtakaye. Na hakuna ajuaye majeshi ya Rabb wako isipokuwa Yeye Pekee. Na haya si chochote isipokuwa ni ukumbusho kwa binaadam.[8]

 

 

كَلَّا وَالْقَمَرِ﴿٣٢﴾

32. Laa, hasha! Naapa kwa mwezi.

 

 

وَاللَّيْلِ إِذْ أَدْبَرَ﴿٣٣﴾

33. Na Naapa kwa usiku unapoondoka.

 

 

وَالصُّبْحِ إِذَا أَسْفَرَ﴿٣٤﴾

34. Na Naapa kwa asubuhi inapoangaza.

 

 

إِنَّهَا لَإِحْدَى الْكُبَرِ﴿٣٥﴾

35. Hakika huo (moto) bila shaka ni mojawapo ya majanga makubwa kabisa.

 

 

 

نَذِيرًا لِّلْبَشَرِ﴿٣٦﴾

36. Ni onyo kwa binaadam.

 

 

 

لِمَن شَاءَ مِنكُمْ أَن يَتَقَدَّمَ أَوْ يَتَأَخَّرَ﴿٣٧﴾

37. Kwa atakaye miongoni mwenu atakadamu mbele au ataakhari nyuma.

 

 

 

كُلُّ نَفْسٍ بِمَا كَسَبَتْ رَهِينَةٌ﴿٣٨﴾

38. Kila nafsi iko katika rehani kwa yale iliyoyachuma.

 

 

إِلَّا أَصْحَابَ الْيَمِينِ﴿٣٩﴾

39. Isipokuwa watu wa kuliani.

 

 

فِي جَنَّاتٍ يَتَسَاءَلُونَ﴿٤٠﴾

40. Katika Jannaat wanaulizana.

 

 

عَنِ الْمُجْرِمِينَ﴿٤١﴾

41. Kuhusu wahalifu.

 

 

مَا سَلَكَكُمْ فِي سَقَرَ﴿٤٢﴾

42. (Watawauliza): Nini kilichokuingizeni katika Saqar?

 

 

 

قَالُوا لَمْ نَكُ مِنَ الْمُصَلِّينَ﴿٤٣﴾

43. Watasema: Hatukuwa miongoni mwa wanaoswali.

 

 

وَلَمْ نَكُ نُطْعِمُ الْمِسْكِينَ﴿٤٤﴾

44. Na wala hatukuwa tunalisha masikini.

 

 

 

وَكُنَّا نَخُوضُ مَعَ الْخَائِضِينَ﴿٤٥﴾

45. Na tulikuwa tunatumbukia kwenye upuuzi pamoja na wanaotumbukia upuuzini.

 

 

 

وَكُنَّا نُكَذِّبُ بِيَوْمِ الدِّينِ﴿٤٦﴾

46. Na tulikuwa tunaikadhibisha Siku ya malipo.

 

 

 

حَتَّىٰ أَتَانَا الْيَقِينُ﴿٤٧﴾

47. Mpaka ikatufikia yakini (mauti).

 

 

 

فَمَا تَنفَعُهُمْ شَفَاعَةُ الشَّافِعِينَ﴿٤٨﴾

48. Basi hautowafaa uombezi wowote wa waombezi.

 

 

 

 

فَمَا لَهُمْ عَنِ التَّذْكِرَةِ مُعْرِضِينَ﴿٤٩﴾

49. Basi wana nini hata wanaugeukilia mbali ukumbusho huu!

 

 

 

 

كَأَنَّهُمْ حُمُرٌ مُّسْتَنفِرَةٌ﴿٥٠﴾

50. Kama kwamba ni punda milia wenye kutimuliwa.

 

 

 

فَرَّتْ مِن قَسْوَرَةٍ﴿٥١﴾

51. Wamekimbia mbio kutokana na wawindaji (au simba).

 

 

 

 

بَلْ يُرِيدُ كُلُّ امْرِئٍ مِّنْهُمْ أَن يُؤْتَىٰ صُحُفًا مُّنَشَّرَةً﴿٥٢﴾

52. Bali anataka kila mtu miongoni mwao wao apewe sahifa zilizofunuliwa.

 

 

 

 

كَلَّا ۖ بَل لَّا يَخَافُونَ الْآخِرَةَ﴿٥٣﴾

53. Laa, hasha! Bali hawaiogopi Aakhirah.

 

 

 

كَلَّا إِنَّهُ تَذْكِرَةٌ﴿٥٤﴾

54. Laa, hasha! Hakika hii (Qur-aan) ni mawaidha. 

 

 

 

فَمَن شَاءَ ذَكَرَهُ﴿٥٥﴾

55. Basi anayetaka atawaidhika.

 

 

 

وَمَا يَذْكُرُونَ إِلَّا أَن يَشَاءَ اللَّـهُ ۚ هُوَ أَهْلُ التَّقْوَىٰ وَأَهْلُ الْمَغْفِرَةِ﴿٥٦﴾

56. Na hawatowaidhika isipokuwa Akitaka Allaah. Yeye Ndiye Mstahiki wa Kuogopwa, na Mstahiki wa Kughufuria (madhambi).

 

 

 

 

 

[1] Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:

 

Bonyeza kiungo kifuatacho:  

 

074-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Muddath-thir Aayah 1-7: يَا أَيُّهَا الْمُدَّثِّرُ

 

[2] Maana Ya Kutoharisha Nguo:

 

Kutoharisha nguo kunawezekana kumaanishwa kutakasa amali kwa kusafishia niyya na kuzitekeleza kwa ukamilifu kabisa, kuondosha chochote ambacho kinaweza kuziharibu na kuzibatilisha kama vile riyaa-a, unafiki, kujisifu, kiburi, uzembe na mengineyo ambayo mtu ameamrishwa kuachana nayo katika ibaada zake.

 

Hayo ni pamoja na kutoharisha nguo za mtu na kuondoa uchafu wake, kwani hiyo ni katika kutakasa amali, khasa katika hali ya Swalaah ambayo ‘Ulamaa wamesema kuwa kuondosha najisi ni katika sharti za Swalaah.

 

Inawezekana pia kwamba kinachokusudiwa ni nguo zake zinazojulikana, na kwamba ameamrishwa kuzitakasa na uchafu wote, wakati wote, na hasa wakati wa kuingia kwenye Swalaah. Na ikiwa ameamrishwa kuitakasa nguo ya nje, basi ni usafi ambao unakamilisha wa ndani. [Tafsiyr As-Sa’diy]

 

Bonyeza viungo vifuatavyo kupata faida zinazohusiana na Twahara ya Swalaah:

 

01-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: كِتَابُ اَلطَّهَارَةِ - Kitabu Cha Twahara

 

[3] Siku Ya Qiyaamah Ni Siku Ngumu Kwa Makafiri:

 

Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى):

  يَقُولُ الْكَافِرُونَ هَـٰذَا يَوْمٌ عَسِرٌ ﴿٨﴾

 Makafiri watasema: Hii ni siku ngumu mno! [Al-Qamar (54:8)]

 

[4] Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:

 

Kuanzia Aayah hii namba (11) hadi namba (31), bonyeza kiungo kifuatacho:  

 

074-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Muddath-thir Aayah 11- 31: ذَرْنِي وَمَنْ خَلَقْتُ وَحِيدًا

 

[5] Alikadiria Vipi?

 

Alipima, alitafakari, alipanga na kuandaa hila ya jinsi ya kumtia dosari Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) na kuibatilisha Qur-aan.  

 

Alitafakari ndani ya nafsi yake akatayarisha la kusema ili kumtukana Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) na Qur-aan, kwa hiyo akalaaniwa na akastahiki kulaaniwa na kuangamizwa kwani vipi alivyojipanga ndani ya nafsi kwa hayo matusi, kisha akalaaniwa tena (Aayah zinazofuatia). [Tafsiyr Al-Muyassar]

 

[6]   سَقَر(Saqar) Na Majina Mengineyo Ya Moto Ya Jahannam:

 

Saqar ni jina miongoni mwa majina ya moto ya Aakhirah, ni moto uwakao vikali mno! Majina mengineyo ya moto ya Aakhirah ni: (i) جَهَنَّم – Jahannam (ii) الجَحِيم – Al-Jahiym (iii) السَّعير -As-Sa’iyr (iv) لَظى – Ladhwaa (v) الْحُطَمَةُ – Al-Hutwamah (vi) الهاوِية – Al-Haawiyah.

 

Kila mmoja una sifa yake maalumu. Baadhi yake Allaah (سبحانه وتعالى)  Ameeleza sifa zake katika Aayah zake zinazoendelea. Na katika majina hayo ya moto, uliotajwa mara nyingi zaidi katika Qur-aan ni Jahannam kama katika An-Nabaa  (78:21), na Al-Jahiym katika An-Naazi’aat (79:36), na As-Sa’iyr katika Al-Inshiqaaq (84:12). Ama mingineyo ni Al-Hutwamah katika Al-Humazah (104:4-5), na Ladhwaa katika Al-Ma’aarij (70: 15-16), na Al-Haawiyah katika Al-Qaari’ah (101: 9-11).

 

Na milango ya moto ni saba kama ilivyotajwa katika Suwrah Al-Hijr (15:44).

 

Rejea An-Nabaa (78:21) kwenye maelezo bayana kuhusu mateso na adhabu za watu wa motoni.

 

[7] Nyoyo Zenye Maradhi:

 

Rejea Suwrah Muhammad (47:20) kwenye maelezo na rejea mbalimbali kuhusu nyoyo zenye maradhi.

 

Rejea pia Al-Hajj (22:46) kwenye maelezo kuhusu maana ya moyo uliopofuka.

 

Rejea pia Ash-Shu’araa (26:88-89) kwenye ufafanuzi na maelezo kuhusu moyo uliosalimika.

 

[8] Tafsiyr Ya Aayah:

 

Na Hatukuwafanya washika hazina wa motoni isipokuwa miongoni mwa Malaika washupavu. Na Hatukuiweka idadi hiyo isipokuwa kuwatahini wale waliomkufuru Allaah na ili imaan ya yakini ipatikane kwa wale Mayahudi na Manaswara waliopewa Vitabu kwamba yaliyokuja ndani ya Qur-aan juu ya washika hazina wa motoni ni ukweli utokao kwa Allaah (سبحانه وتعالى) kwani hayo yanaafikiana na vitabu vyao, na ili Waumini wazidi kumuamini Allaah na Rasuli Wake, na waifuate Sharia Yake kivitendo, na ili wasilifanyie shaka hilo wale Mayahudi na Manaswara waliopewa Vitabu wala wale wenye kumuamini Allaah na Rasuli Wake, na ili wapate kusema wale wenye unafiki ndani ya nyoyo zao na makafiri:  Ni lipi alilolikusudia Allaah kwa idadi hii ya ajabu? Kwa mfano wa hayo yaliyotajwa, Allaah Anampoteza Anayetaka kumpoteza na Anamuongoza Anayetaka kumuongoza. Na hakuna ajuwaye idadi ya askari wa Rabb wako, na miongoni mwao ni Malaika, isipokuwa Allaah Peke Yake. Na haukuwa huu moto isipokuwa ni ukumbusho na mazingatio kwa watu. [Tafsiyr Al-Muyassar]

 

 

 

Share