080 - 'Abasa
عَبَسَ
‘Abasa: 080
080-‘Abasa: Utangulizi Wa Suwrah
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
عَبَسَ وَتَوَلَّىٰ ﴿١﴾
1. Alikunja kipaji na akageuka.[1]
أَن جَاءَهُ الْأَعْمَىٰ ﴿٢﴾
2. Kwa kuwa kipofu alimjia.
وَمَا يُدْرِيكَ لَعَلَّهُ يَزَّكَّىٰ ﴿٣﴾
3. Na nini kitakachokujulisha (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) huenda akatakasika?
أَوْ يَذَّكَّرُ فَتَنفَعَهُ الذِّكْرَىٰ ﴿٤﴾
4. Au atawaidhika na yamfae mawaidha?
أَمَّا مَنِ اسْتَغْنَىٰ ﴿٥﴾
5. Ama yule ajionaye amejitosheleza.
فَأَنتَ لَهُ تَصَدَّىٰ ﴿٦﴾
6. Wewe ndio unamgeukia kumshughulikia!
وَمَا عَلَيْكَ أَلَّا يَزَّكَّىٰ ﴿٧﴾
7. Na si juu yako asipotakasika.
وَأَمَّا مَن جَاءَكَ يَسْعَىٰ ﴿٨﴾
8. Ama yule aliyekujia kwa shime na hima.
وَهُوَ يَخْشَىٰ ﴿٩﴾
9. Naye anakhofu.
فَأَنتَ عَنْهُ تَلَهَّىٰ ﴿١٠﴾
10. Basi wewe unampuuza!
كَلَّا إِنَّهَا تَذْكِرَةٌ ﴿١١﴾
11. Laa hasha! Hakika hizi (Aayah) ni mawaidha.
فَمَن شَاءَ ذَكَرَهُ ﴿١٢﴾
12. Basi atakaye na awaidhike nayo (Qur-aan).
فِي صُحُفٍ مُّكَرَّمَةٍ ﴿١٣﴾
13. Yamo hayo katika Sahifa zenye kuadhimishwa.
مَّرْفُوعَةٍ مُّطَهَّرَةٍ ﴿١٤﴾
14. Zimetukuzwa na zimetakaswa.
بِأَيْدِي سَفَرَةٍ ﴿١٥﴾
15. (Zimebebwa) Mikononi mwa Malaika Wajumbe.[2]
كِرَامٍ بَرَرَةٍ ﴿١٦﴾
16. Watukufu, watiifu.
قُتِلَ الْإِنسَانُ مَا أَكْفَرَهُ ﴿١٧﴾
17. Amelaaniwa na kuangamia binaadamu, ukafiri ulioje alionao?
مِنْ أَيِّ شَيْءٍ خَلَقَهُ ﴿١٨﴾
18. Kutoka kitu gani (Allaah) Amemuumba?
مِن نُّطْفَةٍ خَلَقَهُ فَقَدَّرَهُ ﴿١٩﴾
19. Kutoka tone la manii, Amemuumba, Akamkadiria.
ثُمَّ السَّبِيلَ يَسَّرَهُ ﴿٢٠﴾
20. Kisha Akamuwepesishia njia.
ثُمَّ أَمَاتَهُ فَأَقْبَرَهُ ﴿٢١﴾
21. Kisha Akamfisha, na Akampa takrima ya kuzikwa.
ثُمَّ إِذَا شَاءَ أَنشَرَهُ ﴿٢٢﴾
22. Kisha Atakapotaka, Atamfufua.
كَلَّا لَمَّا يَقْضِ مَا أَمَرَهُ ﴿٢٣﴾
23. Laa hasha! Hakutimiza bado Aliyomuamuru (Allaah).
فَلْيَنظُرِ الْإِنسَانُ إِلَىٰ طَعَامِهِ ﴿٢٤﴾
24. Basi atazame binaadam chakula chake.
أَنَّا صَبَبْنَا الْمَاءَ صَبًّا ﴿٢٥﴾
25. Kwamba Sisi Tumemimina maji kwa uneemefu.
ثُمَّ شَقَقْنَا الْأَرْضَ شَقًّا ﴿٢٦﴾
26. Kisha Tukaipasua ardhi ikafunguka (kwa mimea).
فَأَنبَتْنَا فِيهَا حَبًّا ﴿٢٧﴾
27. Tukaotesha humo nafaka.
وَعِنَبًا وَقَضْبًا ﴿٢٨﴾
28. Na mizabibu na mimea ya mboga (ikatwayo ikamea tena).
وَزَيْتُونًا وَنَخْلًا ﴿٢٩﴾
29. Na mizaituni na mitende.
وَحَدَائِقَ غُلْبًا ﴿٣٠﴾
30. Na mabustani yaliyositawi na kusongamana.
وَفَاكِهَةً وَأَبًّا ﴿٣١﴾
31. Na matunda na majani ya malisho ya wanyama.
مَّتَاعًا لَّكُمْ وَلِأَنْعَامِكُمْ ﴿٣٢﴾
32. Yakiwa ni manufaa kwenu na kwa wanyama wenu wa mifugo.
فَإِذَا جَاءَتِ الصَّاخَّةُ ﴿٣٣﴾
33. Basi utakapokuja ukelele mkali wa kuvuruga masikio.
يَوْمَ يَفِرُّ الْمَرْءُ مِنْ أَخِيهِ ﴿٣٤﴾
34. Siku mtu atakapomkimbia ndugu yake.[3]
وَأُمِّهِ وَأَبِيهِ ﴿٣٥﴾
35. Na mama yake na baba yake.
وَصَاحِبَتِهِ وَبَنِيهِ ﴿٣٦﴾
36. Na mkewe na wanawe.
لِكُلِّ امْرِئٍ مِّنْهُمْ يَوْمَئِذٍ شَأْنٌ يُغْنِيهِ ﴿٣٧﴾
37. Kila mtu miongoni mwao siku hiyo atakuwa na hali yake ya kumtosha mwenyewe.[4]
وُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ مُّسْفِرَةٌ ﴿٣٨﴾
38. Ziko nyuso siku hiyo zitanawiri.[5]
ضَاحِكَةٌ مُّسْتَبْشِرَةٌ ﴿٣٩﴾
39. Zikicheka na kufurahika.
وَوُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ عَلَيْهَا غَبَرَةٌ ﴿٤٠﴾
40. Na ziko nyuso siku hiyo zitakuwa na vumbi juu yake.
تَرْهَقُهَا قَتَرَةٌ ﴿٤١﴾
41. Zitafunikwa na giza totoro.
أُولَـٰئِكَ هُمُ الْكَفَرَةُ الْفَجَرَةُ ﴿٤٢﴾
42. Hao ndio makafiri waovu.
[1] Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah:
Bonyeza kiungo kifuatacho:
080-Asbaabun-Nuzuwl: 'Abasa Aayah 1-10: عَبَسَ وَتَوَلَّىٰ
[2] Fadhila Ya Aliyehifadhi Qur-aan Na Anayeisoma Kwa Kutaabika:
حَدَّثَنَا آدَمُ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، حَدَّثَنَا قَتَادَةُ، قَالَ سَمِعْتُ زُرَارَةَ بْنَ أَوْفَى، يُحَدِّثُ عَنْ سَعْدِ بْنِ هِشَامٍ، عَنْ عَائِشَةَ، عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ " مَثَلُ الَّذِي يَقْرَأُ الْقُرْآنَ وَهْوَ حَافِظٌ لَهُ مَعَ السَّفَرَةِ الْكِرَامِ الْبَرَرَةِ، وَمَثَلُ الَّذِي يَقْرَأُ الْقُرْآنَ وَهْوَ يَتَعَاهَدُهُ وَهْوَ عَلَيْهِ شَدِيدٌ، فَلَهُ أَجْرَانِ ".
Amesimulia ‘Aaishah (رضي الله عنها): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Mfano wa anayesoma Qur-aan hali ameihifadhi, atakuwa pamoja na Malaika Wajumbe, watukufu na watiifu. Na mfano wa anayesoma (Qur-aan), na anaikariri mara kwa mara huku anaona ugumu mkubwa, atapata malipo mawili.” [Al-Bukhaariy Kitabu Cha Tafsiyr (65)]
[3] Siku Ya Qiyaamah Hakuna Ndugu Wala Jamaa Atakayetaka Kumsaidia Ndugu Ya Jamaa Yake:
Rejea Al-Muuminuwn (23:101) Luqmaan (31:33), Al-Muuminuwn (23:101), Faatwir (35:18), Al-Infitwaar (82:19). Rejea pia Al-Hujuraat (49:13) kwenye faida nyenginezo kuhusu maudhui hii.
[4] Kiwewe Cha Siku Ya Qiyaamah Kitamfanya Mtu Asijue Nani Amesimama Karibu Naye:
Siku ya Qiyaamah, watu watafufuliwa wakiwa uchi kama vile walivyozaliwa, na kila mmoja atajali nafsi yake tu! Na kiwewe siku hiyo kitamfanya mtu hata asishughulike kumtazama aliye karibu naye hata kama ni mwanamke au mwanamume! Mama wa Waumini ‘Aaishah (رضي الله عنها) alishtuka aliposikia kuwa hali itakuwa hivyo kama ilivyothibiti katika Hadiyth ifuatayo:
عَنْ عَائِشَةَ (رضي الله عنها) قَالَتْ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: ((يُحْشَرُ النَّاسُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ حُفَاةً عُرَاةً غُرْلا)) قُلْتُ يَا رَسُولَ اللَّهِ، النِّسَاءُ وَالرِّجَالُ جَمِيعًا يَنْظُرُ بَعْضُهُمْ إِلَى بَعْضٍ؟ قَالَ: ((يَا عَائِشَةُ! الأَمْرُ أَشَدُّ مِنْ أَنْ يُهِمَّهُم ذلِكَ)) وَفِي رِواية: ((ألأَمْرُ أَهَمُّ مِنْ أَنْ يَنْظُرَ بَعْضُهُمْ إِلَى بَعْضٍ)) متفق عليه
Amesimulia ‘Aaishah (رضي الله عنها): Nilimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: “Watu watafufuliwa Siku ya Qiyaamah ilhali hawana viatu, wako uchi, ni mazunga (hawakutahiriwa).” Nikamuuliza: Ee Rasuli wa Allaah! Wanaume na wanawake wote watatazamana? Akasema: “Ee ‘Aaishah! Hali itakuwa ngumu mno hata hawatoweza kushughulika na jambo hilo!”
Katika riwaayah nyingine imesema: “Hali itakuwa ngumu mno kiasi kwamba hawatoweza kutazamana.” [Al-Bukhaariy na Muslim]
[5] Nyuso Za Waumini Zitakazonawiri Na Nyuso Za Makafiri Zitakazosawijika:
Aayah hii (38) hadi namba (41) zinataja nyuso za Waumini zitakavyokuwa na nuru kwa furaha ya kufuzu Siku ya Qiyaamah, na nyuso za makafiri zitakavyokuwa na kiza kutokana na huzuni na dhiki.
Anasema hivyo pia Allaah (سبحانه وتعالى) katika Kauli Zake zifuatazo:
يَوْمَ تَبْيَضُّ وُجُوهٌ وَتَسْوَدُّ وُجُوهٌ ۚ فَأَمَّا الَّذِينَ اسْوَدَّتْ وُجُوهُهُمْ أَكَفَرْتُم بَعْدَ إِيمَانِكُمْ فَذُوقُوا الْعَذَابَ بِمَا كُنتُمْ تَكْفُرُونَ ﴿١٠٦﴾ وَأَمَّا الَّذِينَ ابْيَضَّتْ وُجُوهُهُمْ فَفِي رَحْمَةِ اللَّـهِ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿١٠٧﴾
“Siku nyuso zitakuwa nyeupe na nyuso (nyingine) zitakuwa nyeusi. Basi wale ambao nyuso zao zitakuwa nyeusi (wataambiwa): Je, mlikufuru baada ya kuamini kwenu?! Basi onjeni adhabu kwa sababu ya yale mliyokuwa mkiyakanusha. Na wale ambao nyuso zao zitakuwa nyeupe, basi watakuwa katika Rehma ya Allaah. Wao humo watadumu.” [Aal-‘Imraan (3:106-107)]
Na pia kuhusu nyuso za Waumini:
لِّلَّذِينَ أَحْسَنُوا الْحُسْنَىٰ وَزِيَادَةٌ ۖ وَلَا يَرْهَقُ وُجُوهَهُمْ قَتَرٌ وَلَا ذِلَّةٌ ۚ أُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ الْجَنَّةِ ۖ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ﴿٢٦﴾
“Kwa wale waliofanya ihsaan watapata (huko Jannah) jazaa nzuri kabisa na ziada (kumuona Allaah). Na vumbi halitowafunika nyuso zao wala madhila. Hao ni watu wa Jannah, humo wao watadumu.” [Yuwnus (10:26)]
Na pia:
تَعْرِفُ فِي وُجُوهِهِمْ نَضْرَةَ النَّعِيمِ ﴿٢٤﴾
“Utatambua nyuso zao kwa nuru ya neema (taanasa, furaha).” [Al-Mutwaffifiyn (83:21)]
Na pia:
وُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ نَّاعِمَةٌ ﴿٨﴾ لِّسَعْيِهَا رَاضِيَةٌ ﴿٩﴾
“Na nyuso (nyingine) Siku hiyo zitakuwa zenye kuneemeka. Zitafarijika kwa juhudi zake.” [Al-Ghaashiyah (88:8-9)]
Na kuhusu nyuso za makafiri pia:
وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ تَرَى الَّذِينَ كَذَبُوا عَلَى اللَّـهِ وُجُوهُهُم مُّسْوَدَّةٌ ۚ أَلَيْسَ فِي جَهَنَّمَ مَثْوًى لِّلْمُتَكَبِّرِينَ﴿٦٠﴾
“Na Siku ya Qiyaamah utawaona wale waliomsingizia uongo Allaah, nyuso zao zimesawajika. Je, kwani si katika Jahannam ndio makazi kwa ajili ya wanaotakabari?” [Az-Zumar 39:60)]
Na pia:
وُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ خَاشِعَةٌ ﴿٢﴾
“Nyuso siku hiyo zitadhalilika.” [Al-Ghaashiyah (88:2)]