097 - Al-Qadr

 

الْقَدْر

 

097-Al-Qadr

 

 

097-Al-Qadr: Utangulizi Wa Suwrah

 

Alhidaaya.com

 

 

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

 

 

 

إِنَّا أَنزَلْنَاهُ فِي لَيْلَةِ الْقَدْرِ ﴿١﴾

1. Hakika Sisi Tumeiteremsha Qur-aan katika Laylatul-Qadr (Usiku wa Qadr).[1]  

 

 

 

 

وَمَا أَدْرَاكَ مَا لَيْلَةُ الْقَدْرِ ﴿٢﴾

2. Na nini kitakachokujulisha ni nini Laylatul-Qadr?

 

 

 

 

لَيْلَةُ الْقَدْرِ خَيْرٌ مِّنْ أَلْفِ شَهْرٍ ﴿٣﴾

3.  Laylatul-Qadr ni mbora kuliko miezi elfu.

 

 

 

 

تَنَزَّلُ الْمَلَائِكَةُ وَالرُّوحُ فِيهَا بِإِذْنِ رَبِّهِم مِّن كُلِّ أَمْرٍ ﴿٤﴾

4. Wanateremka humo Malaika pamoja na Ar-Ruwh[2] (Jibriyl) kwa Idhini ya Rabb wao kwa kila jambo.

 

 

سَلَامٌ هِيَ حَتَّىٰ مَطْلَعِ الْفَجْرِ ﴿٥﴾

5.  Usiku huo ni amani mpaka kuchomoza Alfajiri.

 

 

 

[1] Al-Qadr:

 

‘Ulamaa wametofautiana kuhusu maana ya neno la القدر  .  Kuna kauli tatu mashuhuri:

 

(i) Al-Qadr ni kwa maana ya التقدير   yaani makadirio (ukadirishaji). Na hapa ina maana kwamba katika usiku huu, makadirio ya mwaka ya viumbe vyote hupitishwa na kukadiriwa. Allaah (سبحانه وتعالى):

فِيهَا يُفْرَقُ كُلُّ أَمْرٍ حَكِيمٍ﴿٤﴾

 

Katika (usiku) huo hupambanuliwa kila jambo la hikmah. [Ad-Dukhaan (44:4)]

 

(ii) Al-Qadr القدر   ni kwa maana ya utukufu na uluwa wa cheo. Hii ina maana kwamba usiku huu una utukufu maalumu kwa Allaah (سبحانه وتعالى).

 

(iii) Al-Qadr  القَدْرُ ni kwa maana ya ufinyu au mbanano. Kwa maana kwamba kutokana na wingi wa Malaika wanaoteremka usiku huo, ardhi inakuwa finyu.

 

 

Tafsiyr zote hizi tatu zinaonyesha ni namna gani usiku huu ulivyo na uzito kwa Allaah (سبحانه وتعالى) kwa Malaika Wake na kwa Waumini.

 

Rejea pia Ad-Dukhaan (44:14) kwenye faida nyenginezo.

 

Bonyeza pia viungo vifuatavyo vyenye faida kuhusu Usiku huu mtukufu, vipi kuupata na fadhila zake:

 

32-Swahiyh Al-Bukhaariy: Kitabu Cha Fadhila Za Layaltul-Qadr: كتاب فضل ليلة القدر

 

35-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Fadhila za Kisimamo cha Usiku wa Qadr (Cheo Kitukufu) na Kubainisha Usiku Unaotarajiwa

 

17-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Mlango Wa Swiyaam: Laylatul Qadr Na Fadhila Zake

 

Laylatul-Qadr- Vipi Uweze Kuupata Usiku Huu?

 

 

18-Hadiyth Za Ramadhwaan Na Mafunzo: Du’aa Usiku Wa Laylatul-Qadr

 

19-Hadiyth Za Ramadhwaan Na Mafunzo: Sifa Za Laylatul-Qadr

 

[2] Maana Za Ruwh Katika Qur-aan:

 

Rejea An-Nahl: (16:2).

 

 

Share