099 - Al-Zalzalah

 

الزَّلْزَلَة

 

099-Al-Zalzalah

 

099-Az-Zalzalah: Utangulizi Wa Suwrah

 

 Alhidaaya.com

 

 

 

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

 

 

 

إِذَا زُلْزِلَتِ الْأَرْضُ زِلْزَالَهَا ﴿١﴾

1. Itakapotetemeshwa ardhi zilzala yake (ya mwisho).[1]

 

 

 

وَأَخْرَجَتِ الْأَرْضُ أَثْقَالَهَا ﴿٢﴾

2. Na itakapotoa ardhi mizigo yake.[2]

 

 

وَقَالَ الْإِنسَانُ مَا لَهَا ﴿٣﴾

3. Na binaadam akasema: Ina nini?

 

 

يَوْمَئِذٍ تُحَدِّثُ أَخْبَارَهَا ﴿٤﴾

4. Siku hiyo itahadithia khabari zake.

 

 

بِأَنَّ رَبَّكَ أَوْحَىٰ لَهَا ﴿٥﴾

5. Kwa kuwa Rabb wako Ameiamuru.

 

 

 

يَوْمَئِذٍ يَصْدُرُ النَّاسُ أَشْتَاتًا لِّيُرَوْا أَعْمَالَهُمْ ﴿٦﴾

6. Siku hiyo watatoka watu makundi mbalimbali wamefarakiana ili waonyeshwe amali zao.[3]

 

 

فَمَن يَعْمَلْ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ خَيْرًا يَرَهُ ﴿٧﴾

7. Basi yule atakayetenda kheri uzito wa chembe (kama atomu) ataiona.

 

 

 

وَمَن يَعْمَلْ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ شَرًّا يَرَهُ ﴿٨﴾

8. Na yule atakayetenda shari uzito wa chembe (kama atomu) ataiona.

 

 


[1] Zilzalah (Tetemeko La Ardhi):

 

‘Ulamaa wamenukuu kauli kadhaa kuhusu zalzalah kama ni Siku ya Qiyaamah au kama zitakithirika kutokea duniani kuwa ni katika alama za kukaribia Qiyaamah. Rejea Al-Hajj (22:1) kwenye maelezo yake.

 

Ikiwa ni Siku ya Qiyaamah, basi siku hiyo itakuwa ngumu mno, kwani zilzalah hiyo itawalewesha watu kutokana na adhabu yake, hata mama mwenye mimba  atazaa mimba yake kama Anavyosema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

يَا أَيُّهَا النَّاسُ اتَّقُوا رَبَّكُمْ ۚ إِنَّ زَلْزَلَةَ السَّاعَةِ شَيْءٌ عَظِيمٌ ﴿١﴾ يَوْمَ تَرَوْنَهَا تَذْهَلُ كُلُّ مُرْضِعَةٍ عَمَّا أَرْضَعَتْ وَتَضَعُ كُلُّ ذَاتِ حَمْلٍ حَمْلَهَا وَتَرَى النَّاسَ سُكَارَىٰ وَمَا هُم بِسُكَارَىٰ وَلَـٰكِنَّ عَذَابَ اللَّـهِ شَدِيدٌ ﴿٢﴾

 

Enyi watu! Mcheni Rabb wenu. Hakika zilizala la Saa ni jambo kuu. Siku mtakapoiona, kila mnyonyeshaji atamsahau anayemnyonyesha, na kila mwenye mimba ataizaa mimba yake, na utawaona watu wamelewa, kumbe hawakulewa lakini ni Adhabu ya Allaah kali! [Al-Hajj (22:1-2)]

 

Na Hadiyth ifuatayo inayothibitisha kuwa ni Qiyaamah:

 

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ بَشَّارٍ، حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ سَعِيدٍ، حَدَّثَنَا هِشَامُ بْنُ أَبِي عَبْدِ اللَّهِ، عَنْ قَتَادَةَ، عَنِ الْحَسَنِ، عَنْ عِمْرَانَ بْنِ حُصَيْنٍ، قَالَ كُنَّا مَعَ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم فِي سَفَرٍ فَتَفَاوَتَ بَيْنَ أَصْحَابِهِ فِي السَّيْرِ فَرَفَعَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم صَوْتَهُ بِهَاتَيْنِ الآيَتَيْنِ أَيُّهَا النَّاسُ اتَّقُوا رَبَّكُمْ إِنَّ زَلْزَلَةَ السَّاعَةِ شَيْءٌ عَظِيمٌ ‏)‏ إِلَى قَوْلِهِ ‏:‏ ‏(‏ إن عذَابَ اللَّهِ شَدِيدٌ ‏)‏ فَلَمَّا سَمِعَ ذَلِكَ أَصْحَابُهُ حَثُّوا الْمَطِيَّ وَعَرَفُوا أَنَّهُ عِنْدَ قَوْلٍ يَقُولُهُ فَقَالَ ‏"‏ هَلْ تَدْرُونَ أَىُّ يَوْمٍ ذَلِكَ ‏"‏ ‏.‏ قَالُوا اللَّهُ وَرَسُولُهُ أَعْلَمُ ‏.‏ قَالَ ‏"‏ ذَاكَ يَوْمٌ يُنَادِي اللَّهُ فِيهِ آدَمَ فَيُنَادِيهِ رَبُّهُ فَيَقُولُ يَا آدَمُ ابْعَثْ بَعْثَ النَّارِ ‏.‏ فَيَقُولُ يَا رَبِّ وَمَا بَعْثُ النَّارِ فَيَقُولُ مِنْ كُلِّ أَلْفٍ تِسْعُمِائَةٍ وَتِسْعَةٌ وَتِسْعُونَ إِلَى النَّارِ وَوَاحِدٌ فِي الْجَنَّةِ ‏"‏ ‏.‏ فَيَئِسَ الْقَوْمُ حَتَّى مَا أَبْدَوْا بِضَاحِكَةٍ فَلَمَّا رَأَى رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم الَّذِي بِأَصْحَابِهِ قَالَ ‏"‏ اعْمَلُوا وَأَبْشِرُوا فَوَالَّذِي نَفْسُ مُحَمَّدٍ بِيَدِهِ إِنَّكُمْ لَمَعَ خَلِيقَتَيْنِ مَا كَانَتَا مَعَ شَيْءٍ إِلاَّ كَثَّرَتَاهُ يَأْجُوجُ وَمَأْجُوجُ وَمَنْ مَاتَ مِنْ بَنِي آدَمَ وَبَنِي إِبْلِيسَ ‏"‏ ‏.‏ قَالَ فَسُرِّيَ عَنِ الْقَوْمِ بَعْضُ الَّذِي يَجِدُونَ ‏.‏ فَقَالَ ‏"‏ اعْمَلُوا وَأَبْشِرُوا فَوَالَّذِي نَفْسُ مُحَمَّدٍ بِيَدِهِ مَا أَنْتُمْ فِي النَّاسِ إِلاَّ كَالشَّامَةِ فِي جَنْبِ الْبَعِيرِ أَوْ كَالرَّقْمَةِ فِي ذِرَاعِ الدَّابَّةِ ‏"‏ ‏.‏ قَالَ أَبُو عِيسَى هَذَا حَدِيثٌ حَسَنٌ صَحِيحٌ ‏.‏

 

Amesimulia ‘Imraan bin Huswayn (رضي الله عنه): Tulikuwa pamoja na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) safarini wakati baadhi ya Swahaba wake wanajikongoja nyuma. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akapaza sauti yake akisoma Aayah hizi mbili:

 

 

يَا أَيُّهَا النَّاسُ اتَّقُوا رَبَّكُمْ ۚ إِنَّ زَلْزَلَةَ السَّاعَةِ شَيْءٌ عَظِيمٌ ﴿١﴾ يَوْمَ تَرَوْنَهَا تَذْهَلُ كُلُّ مُرْضِعَةٍ عَمَّا أَرْضَعَتْ وَتَضَعُ كُلُّ ذَاتِ حَمْلٍ حَمْلَهَا وَتَرَى النَّاسَ سُكَارَىٰ وَمَا هُم بِسُكَارَىٰ وَلَـٰكِنَّ عَذَابَ اللَّـهِ شَدِيدٌ ﴿٢﴾

 

Enyi watu! Mcheni Rabb wenu. Hakika zilizala la Saa ni jambo kuu. Siku mtakapoiona, kila mnyonyeshaji atamsahau anayemnyonyesha, na kila mwenye mimba ataizaa mimba yake, na utawaona watu wamelewa, kumbe hawakulewa lakini ni Adhabu ya Allaah kali! [Al-Hajj (22:1-2)]

 

Swahaba walivyosikia hivyo, wakakimbilia kumfikia kwa sababu walijua kuwa atakuwa ana jambo la kusema. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Mnajua hii ni Siku gani?  Wakasema: Allaah na Rasuli Wake ndio Wajuao zaidi. Akasema: Hiyo ni Siku atakayoitwa Aadam. Rabb wake atamwita na kumwambia: Ee Aadam, walete mbele watu watakaopelekwa motoni. Atasema: Ee Rabb wangu, ni wangapi wa kupelekwa motoni? Atasema: Katika kila elfu moja kuna mia tisa na tisini na tisa wa motoni, na mmoja wa Jannah (Peponi).  Watu wakakata tamaa hadi wakawa hawatabasamu tena. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alipoona hali zao hivyo akasema: “Fanyeni juhudi kutenda (mema) na pokeeni bishara njema, kwani Naapa kwa Ambaye nafsi ya Muhammad imo Mkononi Mwake, nyinyi mtahesabiwa pamoja na viumbe viwili ambao idadi yao ni kubwa mno nao ni Yaajuwj na Maajuwj na wale waliofariki katika kizazi cha Aadam na kizazi cha Ibliys.” Akasema: Basi huzuni za watu zikawaondoka. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: “Fanyeni juhudi na pokeeni bishara njema. Naapa kwa Ambaye nafsi ya Muhammad imo Mkononi mwake! Hakika idadi yenu nyinyi ikilinganishwa na watu (makafiri), si chochote isipokuwa ni kama mfano wa alama ndogo ubavuni mwa ngamia au sehemu isiyo na manyoya kwenye mkono wa mnyama.” [At-Tirmidhiy – Hadiyth Hasan Swahiyh]

 

Na ikiwa ni katika alama za Qiyaamah (tetemeko la ardhi), basi Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ametujulisha hilo pamoja na matukio mengineyo katika Hadiyth ifuatayo:

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، قَالَ قَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم ‏ "‏ لاَ تَقُومُ السَّاعَةُ حَتَّى يُقْبَضَ الْعِلْمُ، وَتَكْثُرَ الزَّلاَزِلُ، وَيَتَقَارَبَ الزَّمَانُ، وَتَظْهَرَ الْفِتَنُ، وَيَكْثُرَ الْهَرْجُ ـ وَهْوَ الْقَتْلُ الْقَتْلُ ـ حَتَّى يَكْثُرَ فِيكُمُ الْمَالُ فَيَفِيضُ ‏"‏‏.‏

 

Amesimulia Abu Hurayrah (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Saa (Qiyaamah) haitatokea hadi Ilmu (ya Dini) itoweke (kwa vifo vya ‘Ulamaa), mitetemeko ya ardhi itatokea mara kwa mara, wakati utapita harakaharaka, fitnah zitadhihirika, mauaji yatakithiri, na mali zitakithirika kwenu na zitazidi mahitaji.”   [Al-Bukhaariy Kitabu Cha Ilmu (15)]

 

[2] Makaburi Yatatoa Viliomo Ndani Yake:

 

Ni sawa na Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):

وَإِذَا الْأَرْضُ مُدَّتْ ﴿٣﴾ وَأَلْقَتْ مَا فِيهَا وَتَخَلَّتْ ﴿٤﴾

 

Na ardhi itakapotandazwa sawa (bila mwinuko wala mwinamo). Na ikatupilia mbali vile vilivyomo ndani yake na ikawa tupu. [Al-Inshiqaaq (84:3-4)

 

Na pia:

 

وَإِذَا الْقُبُورُ بُعْثِرَتْ ﴿٤﴾

Na makaburi yatakapopinduliwa chini juu na kufichuliwa. [Al-Infitwaar (82:4)]

 

 

Wafu na hazina zitatolewa makaburini. [Tafsiyr As-Sa’diy]

 

[3] Watu Watadhihirishiwa Amali Zao Zote Walizozitenda Duniani:

 

Kuanzia Aayah hii namba (6) hadi mwisho wa Suwrah, inathibitishwa kwamba Siku ya Qiyaamah, watu wataonyeshwa matendo yao ya kheri na shari, na kwamba hata tendo liwe dogo vipi litadhihirishwa! Na wala hatoweza mtu kukanusha matendo yake kwa kuwa kila tendo limerekodiwa katika daftari lake. Allaah (سبحانه وتعالى)  Amethibitisha hayo katika Kauli Zake nyingi, miongoni mwazo ni:

عَلِمَتْ نَفْسٌ مَّا قَدَّمَتْ وَأَخَّرَتْ ﴿٥﴾

Nafsi hapo itajua yale iliyoyakadimisha na iliyoyaakhirisha. [Al-Infitwaar (82:5).

 

Na pia:

 

وَوُضِعَ الْكِتَابُ فَتَرَى الْمُجْرِمِينَ مُشْفِقِينَ مِمَّا فِيهِ وَيَقُولُونَ يَا وَيْلَتَنَا مَالِ هَـٰذَا الْكِتَابِ لَا يُغَادِرُ صَغِيرَةً وَلَا كَبِيرَةً إِلَّا أَحْصَاهَا ۚ وَوَجَدُوا مَا عَمِلُوا حَاضِرًا ۗ وَلَا يَظْلِمُ رَبُّكَ أَحَدًا ﴿٤٩﴾

Na kitawekwa Kitabu, basi utaona wahalifu ni wenye khofu kwa yale yaliyomo ndani yake, watasema: Ole wetu! Kitabu hiki kina nini? Hakiachi dogo wala kubwa isipokuwa kimerekodi hesabuni! Na watakuta yale waliyoyatenda yamehudhuria hapo. Na Rabb wako Hamdhulumu yeyote. [Al-Kahf (18:49)]

 

Rejea katika huko kupata rejea nyenginezo mbalimbali.

 

Rejea pia Rejea Al-Israa (17:13-14), Al-Qiyaamah (75:13), At-Takwiyr (81:14). Kote humo kuna faida na rejea nyenginezo za kuthibitisha maudhui hii.

 

 

 

 

Share