101 - Al-Qaari-'ah
الْقَارِعَة
101-Al-Qaari’ah
101-Al-Qaari’ah: Utangulizi Wa Suwrah
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
الْقَارِعَةُ ﴿١﴾
1. Al-Qaari’ah (janga kuu linalogonga).
مَا الْقَارِعَةُ ﴿٢﴾
2. Ni nini hiyo Al-Qaari’ah?
وَمَا أَدْرَاكَ مَا الْقَارِعَةُ ﴿٣﴾
3. Na nini kitakachokujulisha ni nini hiyo Al-Qaari’ah?
يَوْمَ يَكُونُ النَّاسُ كَالْفَرَاشِ الْمَبْثُوثِ ﴿٤﴾
4. Siku watakapokuwa watu kama vipepeo vilivyotawanyika.
وَتَكُونُ الْجِبَالُ كَالْعِهْنِ الْمَنفُوشِ ﴿٥﴾
5. Na majabali yatakuwa kama sufi iliyochambuliwa.
فَأَمَّا مَن ثَقُلَتْ مَوَازِينُهُ ﴿٦﴾
6. Basi yule itakayekuwa mizani yake nzito.[1]
فَهُوَ فِي عِيشَةٍ رَّاضِيَةٍ ﴿٧﴾
7. Basi huyo atakuwa katika maisha ya kuridhisha.
وَأَمَّا مَنْ خَفَّتْ مَوَازِينُهُ ﴿٨﴾
8. Na yule itakayekuwa mizani yake khafifu.
فَأُمُّهُ هَاوِيَةٌ ﴿٩﴾
9. Basi makazi yake ni Haawiyah.[2]
وَمَا أَدْرَاكَ مَا هِيَهْ ﴿١٠﴾
10. Na nini kitakachokujulisha ni nini hiyo Haawiyah?
نَارٌ حَامِيَةٌ ﴿١١﴾
11. Ni moto uwakao vikali mno![3]
[1] Mizani Nzito Na Mizani Nyepesi Za Matendo Ya Wanaadam:
Aayah hii namba (6) hadi (8) zinataja mizani nzito na nyepesi za amali za wanaadam, zitakazopimwa Siku ya Qiyaamah. Wale ambao amali zao njema zitakuwa ni nyingi na za kumridhisha Allaah, basi mizani zao zitakuwa nzito, na hivyo basi watakuwa na maisha ya kuridhisha Peponi. Ama ambao amali zao njema zitakuwa kidogo kutokana na madhambi yao, basi mizani zao zitakuwa nyepesi, na hivyo watakuwa waliokula khasara Aakhirah. Hizo ni sawa na Kauli za Allaah (سبحانه وتعالى):
فَمَن ثَقُلَتْ مَوَازِينُهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ ﴿١٠٢﴾ وَمَنْ خَفَّتْ مَوَازِينُهُ فَأُولَـٰئِكَ الَّذِينَ خَسِرُوا أَنفُسَهُمْ فِي جَهَنَّمَ خَالِدُونَ ﴿١٠٣﴾
Basi yule ambaye mizani yake itakuwa nzito, hao ndio wenye kufaulu. Na yule ambaye mizani zake zitakuwa khafifu, basi hao ni wale ambao wamekhasirika nafsi zao. Watadumu ndani ya Jahannam. [Al-Muuminuwn (23:102-103)]
Na pia Kauli Zake Allaah (سبحانه وتعالى):
وَالْوَزْنُ يَوْمَئِذٍ الْحَقُّ ۚ فَمَن ثَقُلَتْ مَوَازِينُهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ ﴿٨﴾ وَمَنْ خَفَّتْ مَوَازِينُهُ فَأُولَـٰئِكَ الَّذِينَ خَسِرُوا أَنفُسَهُم بِمَا كَانُوا بِآيَاتِنَا يَظْلِمُونَ ﴿٩﴾
Upimaji wa haki utathibiti Siku hiyo. Basi ambao mizani zao zitakuwa nzito, hao ndio watakaofaulu. Na ambao mizani zao zitakuwa khafifu, basi hao ni wale waliojikhasiri wenyewe kwa sababu ya kutozitendea haki Aayaat (na Ishara, Dalili, Hoja) Zetu. [Al-A’raaf (7:8-9)]
Miongoni mwa yanayofanya mizani za amali kuwa nzito:
a-Kumdhukuru Allaah (سبحانه وتعالى) kwa Adkhaar zifuatazo kama alivyosema Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kwamba zinajaza mizani za kupimiwa amali, au zinafanya mizani hizo kuwa nzito:
(i) Kalimah ya لا إلهَ إلَّا اللهُ:
عن ثوبان رضي الله عنه قال : قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : ((بَخٍ بَخٍ لِخمسٍ ما أثقلَهُنَّ في الميزانِ : لا إلهَ إلَّا اللهُ، وسبحانَ اللهِ، والحمدُ للهِ ، واللهُ أكبرُ، والولَدُ الصالِحُ يُتوَفَّى للمرْءِ المسلِمِ فيَحتَسِبُهُ)) النسائي وابن حبان والحاكم ، وأحمد ، وصححه الألباني في صحيح الترغيب والجامع
Amesimulia Thawbaan (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Heko, heko kwa vitu vitano, uzito ulioje vitakavyokuwa nao katika Mizani:
لا إلهَ إلَّا اللهُ، وسبحانَ اللهِ، والحمدُ للهِ ، واللهُ أكبرُ
Laa Ilaaha Illa Allaah, Subhaanah-Allaah, AlhamduliLLah, Allaahu Akbar, na mtoto mwema atakayekufa na wazazi wake wanatarajia thawabu kutoka kwa Allaah.” [An-Nasaaiy, Ibn Hibbaan, Al-Haakim, Ahmad, na Al-Albaaniy kaisahihisha katika Swahiyh At-Targhiyb (1557), Swahiyh Al-Jaami'(2817)]
pia:
عن عبد الله بن عمرو: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: ((إنَّ نبيَّ اللهِ نوحًا لما حضَرَتْه الوفاةُ قال لابنِه: إني قاصٌّ عليك الوصيَّةَ، آمرُك باثنتَينِ و أنهاك عن اثنتَينِ، آمرُك ب ( لاإله إلا اللهُ )، فإنَّ السمواتِ السبعَ والأرَضينَ السبعَ لو وُضِعَتْ في كِفَّةٍ، ووُضِعَتْ لا إلهَ إلا اللهُ في كِفَّةٍ، رجَحَتْ بهنَّ لا إلهَ إلا اللهُ، ولو أنَّ السمواتِ السبعَ والأرَضَينَ السبعَ كُنَّ حَلْقةً مُبهَمةً قصَمَتْهنَّ لا إلهَ إلا اللهُ،
Amesimulia ‘Abdullaah Bin ‘Amr (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Mauti yalipomfikia Nabiy wa Allaah (ambaye ni) Nuwh (عليه السّلام), alimwambia mwanawe: Nakuhadithia wasiya wangu. Nakuamrisha mambo mawili na kukukataza mawili. Nakuamrisha Laa ilaaha illa Allaah (Hapana mwabudiwa wa haki illa Allaah), kwani ingelikuwa mbingu saba na ardhi saba zimewekwa katika mizani na Laa ilaaha illa Allaah imewekwa katika mizani ya pili, basi Laa ilaaha illa Allaah ingelikuwa nzito.
Na kama ingelikuwa mbingu saba na ardhi saba zimefungwa katika mduara, basi Laa illa Allaah ingelivunja mduara huo. [As-Silsilah Asw-Swahiyhah (134)]
(ii) Kumsabihi Allaah kwa سُبْحَانَ اللَّهِ العَظِيمِ، سُبْحَانَ اللَّهِ وَبِحَمْدِهِ
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: " كَلِمَتَانِ خَفِيفَتَانِ عَلَى اللِّسَانِ، ثَقِيلَتَانِ فِي المِيزَانِ، حَبِيبَتَانِ إِلَى الرَّحْمَنِ: سُبْحَانَ اللَّهِ العَظِيمِ، سُبْحَانَ اللَّهِ وَبِحَمْدِهِ " رواه البخاري ومسلم
Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Maneno mawili ni mepesi mno kwa ulimi, mazito mno katika mizani, yanapendeza mno mbele ya Ar-Rahmani (Mwenye kurehemu) nayo ni:
سُبْحَانَ اللهِ العَظِيمِ سُبْحانَ اللهِ وَبِحَمْدِهِ
Subhaana-Allaahil-‘Adhwiym, Subhaana-Allaahi wa-Bihamdihi
Ametakasika Allaah Aliye Mtukufu, Ametakasika Allaah na Himdi ni Zake” [Al-Bukhaariy, Muslim]
“Ametakasika Allaah Mtukufu, Ametakasika Allaah Aliye Mtukufu” [Al-Bukhaariy, Muslim]
(iii) Kumsabbih Allaah kwa سبحانَ اللهِ، والحمدُ للهِ ، واللهُ أكبرُ،
Rejea nukta namba (i) moja juu. Na pia:
عن أبي مالكٍ الحارِثِ بنِ عاصِمٍ الأَشْعَرِيِّ رضي اللهُ عنهُ قال : قال رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم: ((الطُّهُورُ شَطْرُ الإِيَمانِ، والحمدُ لِلهِ تَمْلأُ الْمِيزَانَ، وسُبْحانَ اللهِ والحمدُ لِلهِ تَمْلآنِ - أو تَمْلأُ - ما بَيْنَ السَّمآءِ والأرضِ، والصَّلاةُ نورٌ، والصَّدَقَةُ بُرْهانٌ، والصَّبْرُ ضِيَاءٌ، والْقُرآنُ حُجَّةٌ لَكَ أو عَلَيْكَ، كُلُّ النَّاسِ يَغْدو، فَبائعٌ نَفْسَهُ، فَمُعْتِقُها أَو مُوبِقُها)) رَوَاهُ مُسْلِمٌ
Amesimulia Abuu Maalik Al-Haarith bin ‘Aaswim Al-Ash’ariyy (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Twahaara ni nusu ya imaan, na AlhamduliLLaah inajaza mizani, na Subhaana-Allaah wal-HamduliLLaah inajaza baina ya mbingu na ardhi. Na Swalaah ni nuru, na swadaqa ni burhani na subira ni mwangaza, na Qur-aan ni hoja kwako au dhidi yako. Kila mtu anaianza siku yake akiichuuza nafsi yake, aidha huiokoa ikasalimika au akaiangamiza.” [Muslim]
b-Baadhi ya Adhkaar nyenginezo ambazo thawabu zake ni tele:
i) Kusoma Suwrah Al-Ikhlaasw mara tatu kwa sababu, malipo ya kuisoma Suwrah hii ni sawa na thuluthi ya Qur-aan. Rejea fadhila za Suwrah hii katika utangulizi wa Suwrah. Pia kusoma Suwrah Al-Kaafiruwn kwa kuwa malipo ya kuisoma ni sawa na robo ya Qur-aan. Rejea fadhila za Suwrah hii katika utangulizi wa Suwrah.
ii) Kumsabbih Allaah kwa:
سُبْحـانَ اللهِ وَبِحَمْـدِهِ عَدَدَ خَلْـقِه ، وَرِضـا نَفْسِـه ، وَزِنَـةَ عَـرْشِـه ، وَمِـدادَ كَلِمـاتِـه
Subhaana-Llaahi wa Bihamdihi 'Adada Khalqihi wa Ridhwaa Nafsihi, wa Zinata 'Arshihi wa Midaada Kalimaatih (mara tatu)
Namtakasa Allaah (na kila sifa hasi) na namhimidi kwa idadi ya Viumbe Vyake, na kwa idadi ya vilivyoridhiwa na Nafsi Yake, na kwa uzito wa ‘Arshi Yake, na kwa wingi wa wino wa (kuandikia) Maneno Yake.
Hadiyth ifuatayo imethibiti:
عن أم المؤمنين جُويْريَةَ بنت الحارِث رَضِيَ اللهُ عنها: أنَّ النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم خرجَ مِنْ عِنْدِهَا بُكْرَةً حِيْنَ صَلَّى الصُّبْحَ وَهِيَ في مَسْجِدِها ، ثُمَّ رَجَعَ بَعدَ أنْ أضْحَى وَهِيَ جَالِسَةٌ ، فقالَ : (( مَا زِلْتِ عَلَى الحالِ الَّتي فَارقَتُكِ عَلَيْهَا ؟ )) قالت : نَعَمْ ، فَقَالَ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم : (( لَقَدْ قُلْتُ بَعْدَكِ أرْبَعَ كَلِمَاتٍ ثَلاثَ مَرَّاتٍ ، لَوْ وُزِنَتْ بِمَا قُلْتِ مُنْذُ اليَوْمِ لَوَزَنَتْهُنَّ : سُبْحَانَ الله وَبِحَمْدِهِ عَدَدَ خَلْقِهِ ، وَرِضَا نَفْسِهِ ، وَزِنَةَ عَرْشِهِ ، وَمِدَادَ كَلِمَاتِهِ )) . رواه مسلم
Amesimulia Mama wa Waumini Juwayriyah bint Al-Haarith (رضي الله عنها): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alitoka chumbani kwake mapema pindi aliposwali Swalaah ya Asubuhi, naye (Juwayriyah) alikuwa akiswali. Baadae Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alirudi baada ya kuswali Swalaah ya Dhuwhaa, naye (Juwayriyah) alikuwa bado ameketi (katika mswala wake). Akasema: "Bado upo katika hali ile ile niliyokuacha nayo?" Nikasema: Naam. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: "Hakika baada ya kuondoka nimesema maneno manne mara tatu, lau zitapimwa na kufananishwa na yale uliyosema asubuhi ya leo basi zitakuwa ni nzito zaidi:
سُبْحَانَ الله وَبِحَمْدِهِ عَدَدَ خَلْقِهِ ، وَرِضَا نَفْسِهِ ، وَزِنَةَ عَرْشِهِ ، وَمِدَادَ كَلِمَاتِهِ
Namtakasa Allaah (na kila sifa hasi) na namhimidi kwa idadi ya Viumbe Vyake, na kwa idadi ya vilivyoridhiwa na Nafsi Yake, na kwa uzito wa ‘Arshi Yake, na kwa wingi wa wino wa (kuandikia) Maneno Yake. [Muslim]
c-Kuwa na khulqa (tabia) njema:
عَنْ أَبِي اَلدَّرْدَاءِ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صلى الله عليه وسلم {مَا مِنْ شَيْءٍ فِي اَلْمِيزَانِ أَثْقَلُ مِنْ حُسْنِ اَلْخُلُقِ} أَخْرَجَهُ أَبُو دَاوُدَ، وَاَلتِّرْمِذِيُّ وَصَحَّحَهُ
Amesimulia Abuu Ad-Dardaa (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Hakuna jambo zito katika mizani ya Muumini (Siku ya Qiyaamah) kama khulqa (tabia) njema.” [Imetolewa na Abuu Daawuwd na At-Tirmidhiy na akaisahihisha]
d-Kusindikiza jeneza na kumswalia maiti:
عن ابي هُرَيْرَةَ ـ رضى الله عنه ـ قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم " مَنْ شَهِدَ الْجَنَازَةَ حَتَّى يُصَلِّيَ عَلَيْهَا فَلَهُ قِيرَاطٌ، وَمَنْ شَهِدَ حَتَّى تُدْفَنَ كَانَ لَهُ قِيرَاطَانِ ". قِيلَ وَمَا الْقِيرَاطَانِ قَالَ " مِثْلُ الْجَبَلَيْنِ الْعَظِيمَيْنِ ".
Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Nimemsikia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: “Yeyote anayeusindikiza msafara wa jeneza hadi akaiswalia maiti, basi atapata qiratw moja, na yeyote anayeusindikiza hadi atakapozikwa, basi atapata qiratw mbili.” Likaulizwa swali: Qiratw mbili ndiyo nini? Akajibu: “Ni kama milima mikubwa miwili.” [Al-Bukhaariy Kitabu Cha Jeneza (23)]
Miongoni Mwa Yanayofanya Mizani Kuwa Nyepesi:
i) Dhulma: Anayedhulumu watu kwa mali, ghiybah (kusengenya), kuvunja heshima za watu n.k anakuwa muflis kwa sababu amali zake njema zitachukuliwa na kugaiwa kwa wale aliowadhulumu:
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((أَتَدْرُونَ مَا الْمُفْلِسُ؟)) قَالُوا: الْمُفْلِسُ فِينَا مَنْ لاَ دِرْهَمَ لَهُ وَلاَ مَتَاعَ . فَقَالَ: ((إِنَّ الْمُفْلِسَ مِنْ أُمَّتِي يَأْتِي يَوْمَ الْقِيَامَةِ بِصَلاَةٍ وَصِيَامٍ وَزَكَاةٍ وَيَأْتِي قَدْ شَتَمَ هَذَا وَقَذَفَ هَذَا وَأَكَلَ مَالَ هَذَا وَسَفَكَ دَمَ هَذَا وَضَرَبَ هَذَا فَيُعْطَى هَذَا مِنْ حَسَنَاتِهِ وَهَذَا مِنْ حَسَنَاتِهِ فَإِنْ فَنِيَتْ حَسَنَاتُهُ قَبْلَ أَنْ يُقْضَى مَا عَلَيْهِ أُخِذَ مِنْ خَطَايَاهُمْ فَطُرِحَتْ عَلَيْهِ ثُمَّ طُرِحَ فِي النَّارِ)) مسلم
Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliuliza: “Je, mnamjua muflis? (Swahaba) wakasema: Muflis kwetu sisi ni yule miongoni mwetu asiyekuwa na dirhamu (pesa) wala vyenye kumnufaisha yeye hapa duniani. Akasema (صلى الله عليه وآله وسلم): “Hakika muflis katika Ummah wangu ni yule atakayekuja Siku ya Qiyaamah na Swalaah, Swiyaam, na Zakaah, lakini amemtusi huyu, amemsingizia huyu kuwa amezini, amekula mali ya huyu, amemwaga damu ya mwingine na amempiga mwengine. Thawabu zake zitapatiwa huyu na yule mpaka zimalizike. Na zinapokwisha, basi madhambi ya hao (aliowadhulumu) atabandikwa nayo, kisha atupwe motoni.” [Muslim]
ii) Shirki ya riyaa-a (kujionyesha) inabatilisha amali:
Rejea pia Al-Maa’uwn (107:6)
iii) Hatari ya kutenda Aliyoyaharamisha Allaah:
عَنْ ثَوْبَانَ، عَنِ النَّبِيِّ ـ صلى الله عليه وسلم ـ أَنَّهُ قَالَ : " لأَعْلَمَنَّ أَقْوَامًا مِنْ أُمَّتِي يَأْتُونَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ بِحَسَنَاتٍ أَمْثَالِ جِبَالِ تِهَامَةَ بِيضًا فَيَجْعَلُهَا اللَّهُ عَزَّ وَجَلَّ هَبَاءً مَنْثُورًا " . قَالَ ثَوْبَانُ : يَا رَسُولَ اللَّهِ صِفْهُمْ لَنَا جَلِّهِمْ لَنَا أَنْ لاَ نَكُونَ مِنْهُمْ وَنَحْنُ لاَ نَعْلَمُ . قَالَ : " أَمَا إِنَّهُمْ إِخْوَانُكُمْ وَمِنْ جِلْدَتِكُمْ وَيَأْخُذُونَ مِنَ اللَّيْلِ كَمَا تَأْخُذُونَ وَلَكِنَّهُمْ أَقْوَامٌ إِذَا خَلَوْا بِمَحَارِمِ اللَّهِ انْتَهَكُوهَا " .
Amesimulia Thawbaan (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Hakika najua watu katika ummah wangu ambao watakuja Siku ya Qiyaamah na matendo mema meupe kama milima ya Tihaamah, lakini Allaah Atayafanya kama chembechembe za vumbi zinazoelea hewani zikitawanyika.” Thawbaan akasema: Ee Rasuli wa Allaah! Tufafanulie hao, ili tusiwe miongoni mwao na hali sisi hatujui. Akasema: “Hao ni ndugu zenu na katika kabila zenu, wakifanya ibaada usiku kama mfanyavyo, lakini ni watu ambao wanapokuwa peke yao, wanaruka mipaka kutenda Aliyoyaharamisha Allaah.” [Swahiyh Ibn Maajah (3442)]
Duaa ya kuomba kujaaliwa mizani kuwa nzito:
035-Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Maombi Bora, Duaa, Kufuzu, Amali, Thawabu, Uhai Mauti, Kuthibitishwa, Mizani Nzito.
[2] Haawiyah Ni Katika Majina Ya Moto Wa Aakhirah:
Rejea Al-Muddath-thir (74:26) kwenye majina mengineyo ya moto wa Aakhirah.
[3] Moto Wa Jahannam Kulingana Na Moto Wa Duniani:
Ametaja Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) katika Hadiyth ifuatayo:
حَدَّثَنَا إِسْمَاعِيلُ بْنُ أَبِي أُوَيْسٍ، قَالَ حَدَّثَنِي مَالِكٌ، عَنْ أَبِي الزِّنَادِ، عَنِ الأَعْرَجِ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ ـ رضى الله عنه ـ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ " نَارُكُمْ جُزْءٌ مِنْ سَبْعِينَ جُزْءًا مِنْ نَارِ جَهَنَّمَ ". قِيلَ يَا رَسُولَ اللَّهِ، إِنْ كَانَتْ لَكَافِيَةً. قَالَ " فُضِّلَتْ عَلَيْهِنَّ بِتِسْعَةٍ وَسِتِّينَ جُزْءًا، كُلُّهُنَّ مِثْلُ حَرِّهَا ".
Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Moto wenu ni sehemu ya sehemu sabiini za moto wa Jahannam.” Akaulizwa: Ee Rasuli wa Allaah! Moto wa duniani ulitosha kuwaadhibia waovu. Akasema: “Moto wa Jahannam una sehemu sitini na tisa zaidi ya moto wa dunia, kila moja ya sehemu hizo, joto lake ni sawa na joto la moto wa dunia.” [Al-Bukhaariy Kitabu Cha Uumbaji (59), Muslim Kitabu Cha Jannah Sifa Za Neema Zake Na Wakaazi Wake (53)]