Imaam Ibn ‘Uthaymiyn: Mioyo Ina Hali Za Ajabu

 
Mioyo In Hali Za Ajabu
 
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
 
 
 
Imaam Muhammad bin Swaalih Al-'Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:
 
- Mara moyo unafungamana na dunia.
 
- Na mara unafungamana na jambo (maalum) la kidunia.
 
- Na mara unafungamana na wanawake na unakuwa hamu yake yote ni wanawake.
 
- Na mara unafungamana na maqasri na majumba na unakuwa ndio hamu yake hapo.
 
- Na mara unafungamana na vipando na magari na hayo ndio yanakuwa hamu yake kuu.
 
- Na mara unakuwa uko pamoja na Allaah ('Azza wa Jalla). Daima unafungamana na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa), na unaona kuwa dunia nzima ni njia ya kumpelekea kumwabudu Allaah na kumtii.
Basi (moyo) unaitumia dunia kwa ajili ya kuhakikisha kuabudiwa Allaah ('Azza wa Jalla), kwa sababu ameumbiwa yeye (hiyo dunia) na wala dunia isimtumie yeye. Na hii ndio hali ya juu (miongoni mwa zile hali ambazo moyo unazigeukia kila mara).
 
 
[Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym ya Shaykh Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)]
 

 

 
Share