08-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Sifa Mbaya Za Washirikina

 

إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيمٌ

 

Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!

 

08- Sifa Mbaya Za Washirikina

 

Alhidaaya.com

 

 

1-  Washirikina ni viumbe waovu kabisa kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

 إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ وَالْمُشْرِكِينَ فِي نَارِ جَهَنَّمَ خَالِدِينَ فِيهَاۚ أُولَـٰئِكَ هُمْ شَرُّ الْبَرِيَّةِ ﴿٦﴾

Hakika wale waliokufuru miongoni mwa watu wa kitabu na washirikina watakuwa katika moto wa Jahannam, ni wenye kudumu humo; hao ndio waovu kabisa wa viumbe. [Al-Bayyinah: 6]

 

 

2-Washirikina ni wapotofu hawana akili kama vile wanyama walivyokuwa hawana akili, bali wapotofu zaidi kuliko wanyama!

 

Kwa sababu wana Aadam wamefadhilishwa kupewa akili kinyume na wanyama, lakini wana Aadam hao wanaomkufuru na kumshirkisha Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) ni wenye kufuata hawaa zao, hawatumii akili zao! Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

 أَرَأَيْتَ مَنِ اتَّخَذَ إِلَـٰهَهُ هَوَاهُ أَفَأَنتَ تَكُونُ عَلَيْهِ وَكِيلًا ﴿٤٣﴾

Je, umemuona yule aliyefanya hawaa yake kuwa ndio mwabudiwa wake?  Je, basi utaweza wewe kuwa ni mdhamini wake?

 

 

أَمْ تَحْسَبُ أَنَّ أَكْثَرَهُمْ يَسْمَعُونَ أَوْ يَعْقِلُونَ ۚ إِنْ هُمْ إِلَّا كَالْأَنْعَامِ ۖ بَلْ هُمْ أَضَلُّ سَبِيلًا ﴿٤٤﴾

Je, unadhania kwamba wengi wao wanasikia au wanatia akilini? Wao si chochote isipokuwa kama wanyama, bali wao wamepotea zaidi njia. [Al-Furqaan: 43-44] 

 

 

3- Washirikina, kwa shirki na kufru zao, wamekuwa ni wenye kula na kustarehe kama wanyama. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

وَالَّذِينَ كَفَرُوا يَتَمَتَّعُونَ وَيَأْكُلُونَ كَمَا تَأْكُلُ الْأَنْعَامُ وَالنَّارُ مَثْوًى لَّهُمْ﴿١٢﴾

Na wale waliokufuru wanastarehe na wanakula kama walavyo wanyama wa mifugo na moto ndio makazi yao. [Muhammad: 12]

 

 

 

4- Washirikina ni vipofu, viziwi, mabubu, hawatumii akili!

 

Washirikina walipokuwa wakiitwa kufuata Uongofu wa Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kufuata Tawhiyd na kuacha kumshirikisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) walikanusha, wakapigiwa mfano kama viziwi, mabubu, vipofu, hawana akili! Kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

 

وَإِذَا قِيلَ لَهُمُ اتَّبِعُوا مَا أَنزَلَ اللَّـهُ قَالُوا بَلْ نَتَّبِعُ مَا أَلْفَيْنَا عَلَيْهِ آبَاءَنَا ۗ أَوَلَوْ كَانَ آبَاؤُهُمْ لَا يَعْقِلُونَ شَيْئًا وَلَا يَهْتَدُونَ﴿١٧٠﴾

Na wanapoambiwa: “Fuateni Aliyoyateremsha Allaah” Husema: “Bali tunafuata tuliyowakuta nayo baba zetu.” Je, japokuwa baba zao walikuwa hawaelewi kitu chochote na wala hawakuongoka?

 

 

 وَمَثَلُ الَّذِينَ كَفَرُوا كَمَثَلِ الَّذِي يَنْعِقُ بِمَا لَا يَسْمَعُ إِلَّا دُعَاءً وَنِدَاءً ۚ صُمٌّ بُكْمٌ عُمْيٌ فَهُمْ لَا يَعْقِلُونَ ﴿١٧١﴾

Na mfano wa wale waliokufuru ni kama mfano wa yule ambaye anapiga kelele kwa ambaye hasikii ila sauti na mwito. Viziwi, mabubu, vipofu kwa hiyo hawatii akilini. [Al-Baqarah: 170-171]

 

 

Na Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

وَلَقَدْ ذَرَأْنَا لِجَهَنَّمَ كَثِيرًا مِّنَ الْجِنِّ وَالْإِنسِ ۖ لَهُمْ قُلُوبٌ لَّا يَفْقَهُونَ بِهَا وَلَهُمْ أَعْيُنٌ لَّا يُبْصِرُونَ بِهَا وَلَهُمْ آذَانٌ لَّا يَسْمَعُونَ بِهَا ۚ أُولَـٰئِكَ كَالْأَنْعَامِ بَلْ هُمْ أَضَلُّ ۚ أُولَـٰئِكَ هُمُ الْغَافِلُونَ﴿١٧٩﴾

Kwa yakini Tumeumba Jahannam kwa ajili ya wengi katika majini na wana Adam. Wana nyoyo, lakini hawafahamu kwazo. Na wana macho, lakini hawaoni kwayo. Na wana masikio, lakini hawasikii kwayo. Hao ni kama wanyama, bali wao ni wapotovu zaidi. Hao ndio walioghafilika. [Al-A’raaf: 179]

 

 

Na ndio maana wakawa viumbe waovu kabisa kwa kuwa hawakutaka kumtii Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipowalingania. Wakabakia katia shirki na kufru zao. Basi hawana kheri yoyote ile mbele ya Allaah. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

وَلَا تَكُونُوا كَالَّذِينَ قَالُوا سَمِعْنَا وَهُمْ لَا يَسْمَعُونَ﴿٢١﴾

Na wala msiwe kama wale waliosema: “Tumesikia”; na hali wao hawasikii.

 

 

إِنَّ شَرَّ الدَّوَابِّ عِندَ اللَّـهِ الصُّمُّ الْبُكْمُ الَّذِينَ لَا يَعْقِلُونَ﴿٢٢﴾

Hakika viumbe viovu kabisa mbele ya Allaah ni viziwi, mabubu ambao hawatumii akili.

 

 

وَلَوْ عَلِمَ اللَّـهُ فِيهِمْ خَيْرًا لَّأَسْمَعَهُمْ ۖ وَلَوْ أَسْمَعَهُمْ لَتَوَلَّوا وَّهُم مُّعْرِضُونَ﴿٢٣﴾

Na kama Allaah Angelijua kuwa wana kheri yoyote ile, basi Angeliwasikilizisha; na kama Angeliwasikilizisha, wangeligeuka nao huku wakipuuza. [Al-Anfaal: 21-23]

 

 

 

5- Washirikina ni watu wa najisi!

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّمَا الْمُشْرِكُونَ نَجَسٌ فَلَا يَقْرَبُوا الْمَسْجِدَ الْحَرَامَ بَعْدَ عَامِهِمْ هَـٰذَا

Enyi walioamini!  Hakika washirikiana ni najisi, basi wasikaribie Al-Masjid Al-Haraam baada ya mwaka wao huu. [At-Tawbah: 28]

 

 

 

6-Imeharamishwa kufunga ndoa na washirikina! Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anaamrisha:

 

وَلَا تَنكِحُوا الْمُشْرِكَاتِ حَتَّىٰ يُؤْمِنَّ ۚ وَلَأَمَةٌ مُّؤْمِنَةٌ خَيْرٌ مِّن مُّشْرِكَةٍ وَلَوْ أَعْجَبَتْكُمْ ۗ وَلَا تُنكِحُوا الْمُشْرِكِينَ حَتَّىٰ يُؤْمِنُوا ۚ وَلَعَبْدٌ مُّؤْمِنٌ خَيْرٌ مِّن مُّشْرِكٍ وَلَوْ أَعْجَبَكُمْ ۗ أُولَـٰئِكَ يَدْعُونَ إِلَى النَّارِ ۖ وَاللَّـهُ يَدْعُو إِلَى الْجَنَّةِ وَالْمَغْفِرَةِ بِإِذْنِهِ ۖوَيُبَيِّنُ آيَاتِهِ لِلنَّاسِ لَعَلَّهُمْ يَتَذَكَّرُونَ ﴿٢٢١﴾

Na wala msiwaoe wanawake washirikina mpaka waamini. Na mjakazi Muumini ni bora kuliko mshirikina japo akikupendezeni. Na wala msiwaozeshe (wanawake wa Kiislamu) wanaume washirikina mpaka waamini. Na mtumwa Muumini ni bora kuliko mshirikina japo akikupendezeni. Hao wanaitia katika moto na Allaah Anaitia katika Al-Jannah na maghfirah kwa idhini Yake. Na Anabainisha Aayaat (na shariy’ah) Zake ili wapate kukumbuka. [Al-Baqarah: 221]

 

 

 

 

 

Share