Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Khatwiyb Kusema "Kimu Swalaah" Baada Ya Khutwbah Ya Ijumaa
Hukmu Ya Khatwiyb Kusema "Kimu Swalaah" Baada ya Khutbah Ya Ijumaa
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
Aliulizwa Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) kuhusiana na kauli ya Khatwiyb, "Na Kimu Swalaah", je, hili limepokewa kutoka kwa Salaf (Wema waliotangulia)?
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) akajibu:
Sijui hili kama limepokelewa kutoka kwa Salaf; nakusudia kauli ya Khatwiyb anapomaliza Khutbah, kusema, "Kimu Swalaah, hakika Swalaah hukataza yaliyo machafu na maovu".
Haimpasi Imaam kusema maneno haya, bali anapomaliza Khutbah, anashuka (kutoka katika Minbar) na kisha hukimiwa Swalaah kama alivyokuwa akifanya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Makhaliyfah wake waongofu.
Na ama hii nyongeza, haikupokelewa kutoka kwa Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), wala kutoka kwa Makhaliyfah wake waongofu, wala kutoka kwa mmoja wa Maimaam; na kwa hali hiyo, hakika hukatazwa neno hilo.
[Fataawa Nuur 'Alaa Ad-Darb]