Imaam Ibn Baaz: Hukmu Ya Anayeswali Ijumaa Pekee Na Kuacha Swalaah Zilizobaki
Hukmu Ya Anayeswali Ijumaa Pekee Na Kuacha Swalaah Zilizobaki
Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah)
SWALI:
Kuna mtu anaswali Ijumaa pekee bila kuswali Fardhi zilizobaki, je, inakubaliwa Swalaah yake?
JIBU:
Haikubaliwi Swalaah yake, kwa hakika amekuwa Kafiri kwa hilo.
Swalaah yake ya Ijumaa, Swawm yake, na matendo yake yote ni batili.
Anasema Aliyetukuka:
"Na kama wangemshirikisha bila shaka yangebatilika yale waliyokuwa wakitenda." [Al-An'aam: 88]
Na Anasema Aliyetakasika:
"Na yeyote atakayekufuru iymaan; basi kwa yakini zimebatilika 'amali zake; naye Aakhirah atakuwa miongoni mwa waliokhasirika." [Al-Maaidah: 5]
Basi yule anayekufuru kufru kubwa au shirki kubwa, huporomoka matendo yake.
Tunamuomba Allaah afya (Atulinde).
Na kuacha Swalaah ni kufru kubwa."
[Nuwr 'Alaa Ad-Darb, 13/339]