Supu Ya Kuku Ya Mboga Na Sosi Ya Beshamel
Supu Ya Kuku Ya Mboga Na Sosi Ya Beshamel
Vipimo
Kuku - ½
Chumvi - kiasi
Pilipili manga - 1 kijiko cha chai
Kiazi - 1
Kiazi kitamu - 1
Brokoli - kipande kiasi
Koliflower (cauliflower) - kipande kiasi
Karoti - 2
Boga - kipande kiasi
Mumunya - kipande kiasi
Uyoga (mushroom) - ½ kikombe
Mahindi machanga (baby corn) - kiasi
Parsely (aina ya kotmiri) - kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na kupika
- Muoshe kuku vizuri, toa ngozi, katakata, kisha weka katika sufuri, tia chumvi, pilipili manga na ndimu.
- Weka maji kiasi ya kutosha yasibakie mengi sana. Chemsha mpaka awive.
- Epua toa nyama kuku kisha toa mifupa, chambua chambua. Ukipenda bakisha mifupa.
- Katakata mboga zote vipande vipande na katakata (chop) parsley
- Weka mboga zote katika supu ya kuku zichemshe ziive kidogo tu.
- Rudisha nyama kuku ulochambua katika supu ichanganyike na mboga.
- Weka sufuria nyengine tengeneza beshamel.
Vipimo Vya Beshamel
Unga - 2 vijiko vya kulia
Siagi - 2 vijiko vya kulia
Maziwa ya unga - 1 gilasi moja
Kidonge cha supu (stock) - 1
Namna ya kutengeneza Beshamel
- Teka supu kiasi gilasi mbili changanya na maziwa.
- Weka siagi katika sufuria, tia unga kaanga mpaka uanze kugeuka rangi.
- Mimina maziwa, tia kidonge cha supu, kisha iache ichemke kiasi.
- Mimina mchanganyiko wa kuku na mboga pamoja na supu kama imebakia kidogo.
- Onja ukolezee kiasi upendavyo.
- Unaweza kupunguza uzito wa beshamel kwa kupunguza maziwa kidogo:
Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)