Shaykh Fawzaan: Fadhila Za Kujifunza ‘Ilmu Ya Shariy’ah (Dini), Na Je Ina Mipaka?
Fadhila Za Kujifunza ‘Ilmu Ya Shariy’ah, Na Je, Ina Mipaka?
Shaykh Swaalih bin Fawzaan Al-Fawzaan (Hafidhwahu Allaah)
SWALI:
Nini Fadhila Za Kujifunza ‘Ilmu Ya Shariy’ah, Na Je, Ina Mipaka?
JIBU:
Naam, kujifunza ‘ilmu ya Shariy’ah (Dini) kwa niyyah njema ni ‘amali bora kabisa.
عَنْ عُثْمَانَ رَضِي اللَّه عَنْه عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((خَيْرُكُمْ مَنْ تَعَلَّمَ الْقُرْآنَ وَعَلَّمَهُ))
Imepokelewa kutoka kwa ‘Uthmaan bin ‘Affaan (Radhwiya Alaahu ‘anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Mbora wenu ni yule anayejifunza Qur-aan kisha akaifundisha))
Na haikusudiwi kuwa kujifunza Qur-aan khasa kwa ajili ya kuihifadhi au kuisoma, bali kujifunza kuifanyia kazi pia, na kuifundisha kwa watu, na kuibainisha, na kubainisha kwa watu maana yake.
Hivi ndivyo kujifunza Qur-aan kwa sababu Qur-aan ndio dalili juu ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa), ndiyo maneno ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) na inatosheleza kwayo kuwa ni maneno ya Allaah Rabb (Mola) wa ulimwengu kuwa ni Mwongozo wetu, na kwa ajili ya kubainisha yanayotufaa, na kujitahadhirsha yale yanayotudhuru, basi Qur-aan utakuta humo yote ni amri au makatazo au khabari; (kuhusu) maamrisho ya utii na makatazo ya kumuasi Allaah au khabari kuhusu ummah za Makafiri waliopita na matokeo yake au khabari kuhusu yatakayotokea zama za mwisho yaliyo ya fitnah na vipi kujiepusha nazo na vipi kujitahadharisha nazo na kutahadharisha wengineo.
[Al-Mawqi' Ar-Rasmiy Li-Ma'aaliy Ad-Duktuwr Swaalih bin Fawzaan...]