Al-Lajnah Ad-Daaimah: Pokemon GO - Fatwa Ya Kale Imejadidishwa
‘Pokemon GO’ - Fatwa Ya Kale Imejadidishwa
Al-Lajnah Ad-Daaimah
Fatwa ya zamani inayohusu mchezo tata unaojulikana kama ‘Pokemon’ ambao mwanzo uliibuka miaka ya tisini na kurudi tena kwa kasi masiku ya karibuni ya mwaka huu wa 1437 H sawa na 2016 M, iliyotolewa na Kamati Ya Kudumu Ya Utafiti Na Utoaji Fatwa imejadidishwa na baraza la Wanachuoni Wakubwa wa Saudia.
Fatwa hiyo imejadidishwa kwenye tovuti ya Utafiti Wa Kielimu Na Utoaji Fatwa.
Fatwa hiyo ya zamani yenye namba 21,758 iliyotolewa mwaka 2001, miaka 15 iliyopita, ambayo katika fatwa hiyo, iliuona mchezo huo una mwelekeo wa Kamari, ambayo ni haraam katika Uislamu.
Shaykh Swaalih Al-Fawzaan (Hafidhwahu Allaah), mjumbe wa Baraza la Wanachuoni Wakubwa, alisema kuwa, muundo mpya wa mchezo huo uliotoka karibuni, ni sawa sawa na ule wa zamani.
Katika fatwa hiyo, inayopatikana alhidaaya
ilieleza mambo mbalimbali yaliyopigwa marufuku yaliyomo kwenye mchezo huo ambayo yanahalalisha kuukataza mchezo huo ambao unahusisha uchezaji Kamari kama ambavyo ndani ya mchezo huo, wachezaji wawili wanashindana kupata kadi nyingi ambazo zina zawadi tofauti. Yule mchezaji mwenye uwezo katika hao wawili ndiye hushinda kwa kupata kadi. Yule aliyeshindwa akikataa kukubali kushindwa, basi analipa ile thamani.
Na makatazo mengine yaliyomo ndani ya mchezo huo ni kule kuwemo ushirikina na iymaan ya kuabudu miungu wengi na kukuza na kutangaza ukafiri, nembo za kishirikina, picha haram na makatazo mengine.
(Mchezo huo umevuruga sana akili za watoto na vijana na kuwashughulisha kupita mipaka).