Mikate Ya Hamira Na Ufuta Ya Kuoka (Baked)
Mikate Ya Hamira Na Ufuta Ya Kuoka (Baked)
Vipimo
Unga - 4 mugs (vikombe vikubwa)
Hamira - 1 Kijiko cha kulia
Mtindi (Yoghurt) - 1 kijiko cha kulia
Yai - 1
Samli - 1 kijiko cha kulia
Tui la nazi au maziwa - 1 ½ mug (takriban)
Chumvi - kiasi
Ufuta - kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Katika bakuli au mashine ya kukandia unga, weka vitu vyote isipokuwa ufuta.
- Kanda vizuri mpaka uwe laini.
- Fanya madonge saizi upendayo yasiwe madogo sana.
- Sukuma kila donge kisha pakaza samli kidogo ukunje kama paratha (chapati za mafuta).
- Pakaza siagi au samli katika treya ya oveni. Panga mikate, kisha iache iumuke.
- Piga yai moja vizuri kisha kisha upakaze kwa brush juu ya mikate na nyunyizia ufuta.
- Oka (bake) katika oveni moto wa kiasi. Ikikaribia kuiva, iwashie moto wa juu kidogo igeuke rangi na kumalizikia kuivisha.
- Epua weka katika sahani, pakaza samli ikiwa tayari.
Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)