079-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Baqarah Aayah 079: فَوَيْلٌ لِّلَّذِينَ يَكْتُبُونَ الْكِتَابَ بِأَيْدِيهِمْ ثُمَّ يَقُولُونَ
أسْبابُ النُّزُول
Asbaabun-Nuzuwl
(Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)
Imekusanywa na: Alhidaaya.com
Al-Baqarah Aayah 79: Basi ole kwa wale wenye kuandika kitabu kwa...
فَوَيْلٌ لِّلَّذِينَ يَكْتُبُونَ الْكِتَابَ بِأَيْدِيهِمْ ثُمَّ يَقُولُونَ هَـٰذَا مِنْ عِندِ اللَّـهِ لِيَشْتَرُوا بِهِ ثَمَنًا قَلِيلًا ۖ فَوَيْلٌ لَّهُم مِّمَّا كَتَبَتْ أَيْدِيهِمْ وَوَيْلٌ لَّهُم مِّمَّا يَكْسِبُونَ ﴿٧٩﴾
79. Basi ole kwa wale wenye kuandika kitabu kwa mikono yao; kisha wakasema: ”Hiki ni kutoka kwa Allaah” ili wabadilishe kwa thamani ndogo. Basi ole wao kwa yale yaliyoandikwa na mikono yao, na ole wao kwa yale wanayoyachuma
Sababun-Nuzuwl:
Aayah hii imeteremka ikiwazungumzia Mayahudi na Manaswara kama ilivyohadithiwa na Al-Bukhaary katika: Khalqu Af-’aal Al-‘Ibaad kutoka kwa Swahaba Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما)]
Na Hadiyth hiyo ameikusanya Al-Bukhaariy katika: Kitaab Al-I’tiswaam bil-Kitaab wa Sunnah kama ifuatavyo:
عَنْ عُبَيْدِ اللَّهِ، أَنَّ ابْنَ عَبَّاسٍ رضى الله عنهما قَالَ كَيْفَ تَسْأَلُونَ أَهْلَ الْكِتَابِ عَنْ شَىْءٍ، وَكِتَابُكُمُ الَّذِي أُنْزِلَ عَلَى رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم أَحْدَثُ، تَقْرَءُونَهُ مَحْضًا لَمْ يُشَبْ وَقَدْ حَدَّثَكُمْ أَنَّ أَهْلَ الْكِتَابِ بَدَّلُوا كِتَابَ اللَّهِ وَغَيَّرُوهُ وَكَتَبُوا بِأَيْدِيهِمُ الْكِتَابَ وَقَالُوا هُوَ مِنْ عِنْدِ اللَّهِ. لِيَشْتَرُوا بِهِ ثَمَنًا قَلِيلاً، أَلاَ يَنْهَاكُمْ مَا جَاءَكُمْ مِنَ الْعِلْمِ عَنْ مَسْأَلَتِهِمْ، لاَ وَاللَّهِ مَا رَأَيْنَا مِنْهُمْ رَجُلاً يَسْأَلُكُمْ عَنِ الَّذِي أُنْزِلَ عَلَيْكُمْ.
Imetoka kwa ‘Ubaydullaah kwamba Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) amesema: “Kwanini mnawauliza Ahlul-Kitaab kuhusu jambo lolote na hali Kitabu chenu (Qur-aan) ambacho kimeteremka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ni cha mwisho? Mnakisoma kikiwa kimetakasika hakikubadilisha wala kupotoshwa na Allaah Amekujulisheni kuwa Ahlul-Kitaab wamebadili Kitabu cha Allaah na wakakibadilisha na wakaandika kwa mikono yao Kitabu kisha wakasema ni kutoka kwa Allaah ili wabadilishe kwa thamani ndogo. Je kwani ilmu iliyokujieni haikukatazeni kuwauliza wao chochote? Hapana, wa-Allaahi hatukumuona mtu yeyote kati yao akikuulizeni yaliyoteremshwa kwenu.”
Na akahadithia pia katika Kitaab Ash-Shahadaat, na Kitaab At-Tawhiyd.