Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Awrah Ya Mwanamke Mbele Ya Mahaarim Wake
‘Awrah Ya Mwanamke Mbele Ya Mahaarim Wake
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
SWALI:
Kipi kiasi kinachochukuliwa kuwa ni 'awrah kwa mwanamke awapo na wajomba zake kwa upande wa mama, wajomba zake upande wa baba na ndugu zake, nyumbani?
JIBU:
Anaruhusiwa kuonyesha kwa Mahram wake: uso, kichwa, shingo, mikono, miguu, chini ya muundi, na anapaswa kusitiri kila kitu mbali na hivyo tulivyotaja.
[Imaam Muhammad bin Swaalih Al-‘Uthaymiyn - Hijaab Al-Mar-ah wa ziynatuhaa, ukurasa wa 43]
