Shaykh Fawzaan: Kuwalea Watoto Kwa Filamu Za Katuni
Kuwalea Watoto Kwa Filamu Za Katuni
Shaykh Swaalih bin Fawzaan Al-Fawzaan (Hafidhwahu Allaah)
SWALI:
Nini hukmu ya kuwalea watoto kwa filamu za katuni kwa lengo kwamba mna faida humo kwamba zinawalea katika akhlaaq (tabia) njema?
JIBU:
Allaah Ameharamisha picha, na Ameharamisha kuzikusanya na kuzihifadhi kama kumbukumbu, basi vipi tuwalee kwazo watoto wetu?
Vipi tuwaleee kwa kitu cha haraam? Kwa picha ambazo zimeharamishwa na visanamu vinavyotaharuki vyenye kuongea kama kumshabihisha bin Aadam? Picha hizi ni mbaya kabisa.
Wala haijuzu kuwalea watoto kwa katuni hizo. Na hayo ndiyo wanayoyataka makafiri kwamba tukhalifu yale aliyokataza Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).
Kwani Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza picha na kuzitumia na kuzihifadhi, na hawa (makafiri) wanayaeneza kwa vijana na kwa Waislamu kwa hoja kuwa ni malezi (mema) na hali malezi hayo ni ya ufisadi.
Malezi mazuri ni kuwafundisha yale yanayowafaa katika Dini yao na dunia yao.
[Majmu’ Rasaail Da’wiyyah wa Manhajiyyah (272)]