20-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Je, Inajuzu kustaghithi (kuomba uokovu) maiti na wasiokuwepo?

 Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com

 

 

 

20-Je, Inajuzu kustaghithi (kuomba uokovu) maiti na wasiokuwepo?

 

Hapana! Haijuzu kustaghithi kwa maiti na wasiokuwepo, bali tustaghithi (tuombe uokovu) kwa Allaah.

 

إِذْ تَسْتَغِيثُونَ رَبَّكُمْ فَاسْتَجَابَ لَكُمْ

Na (kumbukeni) pale mlipomuomba uokovu Rabb wenu Naye Akakuitikieni [Al-Anfaal: 9] 

 

((كَانَ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِذَا أصابه هَمٌّ أَوْ غَمٌّ قَالَ: ((يَا حيُّ يَا قيّوم برحمتك أستغيث))    رواه الترمذي

Alikuwa (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) anapofikwa na wahka au dhiki husema: ((Yaa Hayyu Yaa Qayyuwm bi Rahmatika astaghiythu - Ee Uliye hai daima, Msimamia wa kila kitu, kwa rahmah Zako naomba uokozi)) [At-Tirmidhy Hadiyth Hasan]

 

 

 

 

Share