42-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Nani kiumbe cha mwanzo na kipi kilichoumbwa mwanzo?
Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu
Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.
Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com
42-Nani kiumbe cha mwanzo na kipi kilichoumbwa mwanzo?
Kiumbe cha mwanzo kabisa ni Aadam ('Alayhis-Salaam) na kitu cha mwanzo kuumbwa ni kalamu.
إِذْ قَالَ رَبُّكَ لِلْمَلَائِكَةِ إِنِّي خَالِقٌ بَشَرًا مِّن طِينٍ ﴿٧١﴾
Pale Rabb wako Alipowaambia Malaika: “Hakika Mimi Namuumba mtu kutokana na udongo. [Swaad: 71]
((إنّ أوّلَ مَا خَلَقَ اللهُ الْقَلَم)) رواه أبو داود والترمذي، وقال: حسن صحيح
((Kitu cha kwanza Alichoumba Allaah ni kalamu)) [Abuu Daawuwd, At-Tirmidhiy amesema Hasan Swahiyh]