49-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Je, tutosheke na Qur-aan bila Hadiyth?
Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu
Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.
Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com
49-Je, tutosheke na Qur-aan bila Hadiyth?
Hapana! Tunapaswa tuifuate Qur-aan na pia Hadiyth bila kutosheka na Qur-aan pekee.
وَأَنزَلْنَا إِلَيْكَ الذِّكْرَ لِتُبَيِّنَ لِلنَّاسِ مَا نُزِّلَ إِلَيْهِمْ
(Tumewatuma) Kwa hoja bayana na vitabu. Na Tumekuteremshia Ukumbusho (Qur-aan) ili uwabainishie watu yaliyoteremshwa kwao. [An-Nahl: 44]
((أَلَا إِنِّي أُوتِيتُ الْقُرْآنَ وَمِثْلَهُ مَعَهُ)) صحيح رواه أبو داود
((Hakika mimi nimepewa Qur-aan na mfano wake)) [Hadiyth Swahiyh, Abuu Daawuwd]