53-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Je, Ipo bid'ah inayoitwa bid-‘atun-hasanah’ katika Dini?
Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu
Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.
Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com
53-Je, Ipo bid'ah inayoitwa bid-‘atun-hasanah’ katika Dini?
Hapana! Hakuna bid’atun-hasanah (uzushi mzuri) katika Dini.
الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ وَأَتْمَمْتُ عَلَيْكُمْ نِعْمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمُ الْإِسْلَامَ دِينًا ۚ
Leo Nimekukamilishieni Dini yenu, na Nimekutimizieni neema Yangu, na Nimekuridhieni Uislaam uwe Dini yenu. [Al-Maaidah: 3]
((إِيَّاكُمْ وَمُحْدَثَاتِ الْأُمُورِ، فَإِنَّ كُلَّ مُحْدَثَةٍ بِدْعَةٌ، وَكُلَّ بِدْعَةٍ ضَلَالَةٌ)) صحيح رواه أبو داود
((Jitahadharini na uzushi wa mambo, kwani kila uzushi ni bid'ah na kila bid'ah ni upotofu)) [Swahiyh - Abuu Daawuwd]