15-Wewe Pekee Tunakuabudu: Tawassul Zinazokubalika: Kutawassal Kwa Jina Adhimu Kabisa La Allaah
إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ
Wewe Pekee Tunakuabudu Na Wewe Pekee Tunakuomba Msaada
Tawassul Zinazokubalika
15-Kutawasal Kwa Jina Adhimu (Tukufu) Kabisa La Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)
Hakuna ajuaye Jina Adhimu kabisa la Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa). Lakini Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ametudokezea kama ifuatavyo:
عَنْ الْقَاسِمِ عَنْ أَبِي أُمَامَةَ (رضي الله عنه) عَنْ النَّبِيِّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم)َ: ((اسْمُ اللَّهِ الأَعْظَمُ الَّذِي إِذَا دُعِيَ بِهِ أَجَابَ فِي سُوَرٍ ثَلاَثٍ: الْبَقَرَةِ، وَآلِ عِمْرَانَ، وَطه))
Kutoka kwa Al-Qaasim, kutoka kwa Abuu Umaamaah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Jina Adhimu kabisa la Allaah ambalo likiombewa kwalo Anaitikia, limo katika Suwrah tatu; Al-Baqarah, Aal-‘Imraan, na Twaahaa)) [Swahiyh Ibn Maajah (3124), Swahiyh Al-Jaami’ (979)]
Katika Suwrah hizo Majina mawili ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Ambayo yamelingana kuweko kwa pamoja ni “Al-Hayyu”, “Al-Qayyuwm” na Akayataja tena hayo pamoja na Majina ya Allaah, Ilaah, Al-Waahid, Ar-Rahmaan, Ar-Rahiym:
عَنْ أَسْمَاءَ بِنْتِ يَزِيدَ (رضي الله عنها) أَنَّ النَّبِيَّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) قَالَ: ((اسْمُ اللَّهِ الأَعْظَمُ فِي هَاتَيْنِ الأَيَتَيْنِ ((وَإِلَـٰهُكُمْ إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ ۖ لَّا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الرَّحْمَـٰنُ الرَّحِيمُ)) وَفَاتِحَةِ آلِ عِمْرَانَ ((الم اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّومُ ))
Kutoka kwa Asmaa bint Yaziyd (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Jina Adhimu kabisa la Allaah limo katika Aayah zifuatazo: “Na Ilaah wenu (Allaah) ni Ilaah Mmoja, hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye, Ar-Rahmaan, Mwenye kurehemu.” (Al-Baqarah: 163) na na ufunguo (mwanzo) wa ‘Aal-‘Imraan: “Alif Laam Miym. Allaah, hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye, Aliye hai daima, Msimamia kila kitu. [Aal-‘Imraan: 1-2] [Swahiyh At-Tirmidhiy (3478), Swahiyh Ibn Majaah (3123), Swahiyh Al-Jaami’ (980), Swahiyh Abiy Daawuwd (1496) Swahiyh At-Targhiyb (1642)]
Naye Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiomba du’aa kwa kutaja baadhi ya Majina hayo mfano du’aa yake ambayo alikuwa anapopatwa dhiki au huzuni akiomba:
يَا حَيُّ يَا قَيُّومُ بِرَحْمَتِكَ أَسْتَغِيثُ
“Yaa Hayyu Yaa Qayyuwm bi-Rahmatika astaghiythu”
(Ee Uliye Hai daima, Msimamia wa kila jambo, rahmah Zako naomba uokovu) [At-Tirmidhiy (3524), An-Nasaaiy fiy As-Sunan Al-Kubraa(6/147), Al-Haakim (1/730) na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh At-Tirmidhiy]
Pia akaashiria Majina ya Allaah (Subhaanahuu wa Ta’aala) mengineyo katika Hadiyth:
عن أنس بن مالك (رضي الله عنه) قال: سَمِعَ النَّبِيُّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) رَجُلاً يَقُولُ: ((اللَّهُمَّ إنِّي أسْألُكَ بِأنَّ لَكَ الْحَمْدَلا إِلَهَ إِلاَّ أنْتَ وَحْدَكَ لا شَرِيكَ لَكَ، الْمَنَّانُ، بَدِيعُ السَّمَوَاتِ وَالأرْضِ ذُو الْجَلالِ وَالإِكْرَام)) فقال: ((لَقَدْ سَألَ اللَّهَ بِاسْمِهِ الأعْظَمِ الَّذِي إذَا سُئِلَ بِهِ أعْطَى وَإذَا دُعِيَ بِهِ أجَابَ))
Kutoka kwa Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimsikia mtu akiomba:
اللَّهُمَّ إنِّي أسْألُكَ بِأنَّ لَكَ الْحَمْدَلا إِلَهَ إِلاَّ أنْتَ وَحْدَكَ لا شَرِيكَ لَكَ، الْمَنَّانُ، بَدِيعُ السَّمَوَاتِ وَالأرْضِ ذُو الْجَلالِ وَالإِكْرَام)
“Allaahumma inniy As-alauka bianna Lakal-Hamdu laa ilaaha illa Anta Wahdaka laa shariyka Laka. Al-Mannaanu, Badiy'us-samaawati wal-ardhwi, Dhul-Jalaali wal-Ikraami”
(Ee Allaah hakika mimi nakuomba kwamba Himdi ni Zako, hapana mwabudiwa wa haki ila Wewe, Huna mshirika, Al-Mannaanu (Mwingi wa neema, Mwingi wa kutoa na kutunuku, na kufadhili na kuwafanyia ihsaan waja Wake, Mwanzishi wa mbingu na ardhi, Mwenye Ujalali na Ukarimu”.
Akasema: ((Kwa yakini amemuomba Allaah kwa Jina Lake Adhimu kabisa ambalo Akitakwa jambo kwalo Anatoa na Anapoombwa Huitikia))[Swahiyh Ibn Maajah (3126)]
Na pia akataja Majina mengineyo katika Hadiyth:
عن عَبْدِ اللَّهِ بن بُرَيْدَةَ الأسْلَمِيِّ عن أبِيهِ (رضي الله عنهما) قال: سَمِعَ النَّبِيُّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) رَجُلاً يَدْعُو وَهُوَ يَقُولُ: "اللَّهُمَّ إنِّي أسْأَلُكَ بِأنِّي أشْهَدُ أنَّكَ أنْتَ اللَّهُ لا إِلَهَ إِلاَّ أنْتَ الأحَدُ الصَّمَدُ الَّذِي لَمْ يَلِدْ وَلَمْ يُولَدْ وَلَمْ يَكُنْ لَهُ كُفُوًا أحَدٌ" فقال: ((وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ لَقَدْ سَألَ اللَّهَ بِاسْمِهِ الأعْظَمِ الَّذِي إذَا دُعِيَ بِهِ أجَابَ وَإذَا سُئِلَ بِهِ أعْطَى))
Kutoka kwa ‘Abdullaah bin Buraydah Al-Aslamiyy, kutoka kwa baba yake (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimsikia mtu akiomba:
"اللَّهُمَّ إنِّي أسْأَلُكَ بِأنِّي أشْهَدُ أنَّكَ أنْتَ اللَّهُ لا إِلَهَ إِلاَّ أنْتَ الأحَدُ الصَّمَدُ الَّذِي لَمْ يَلِدْ وَلَمْ يُولَدْ وَلَمْ يَكُنْ لَهُ كُفُوًا أحَدٌ"
“Allaahumma inni as-aluka bianniy ash-hadu Annaka Anta-Allaahu laa ilaaha illa Anta Al-Ahadu Asw-Swamadu, Alladhiy lam Yalid walam Yuwlad walam Yakun Lahuu kufuwan ahad”.
(Ee Allaah, hakika mimi nakuomba kwa kushuhudia kwamba hakika Wewe ni Allaah, hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Wewe, Mmoja, Aliyekamilika sifa za kila aina ya utukufu Wake, Mwenye kukusudiwa kwa haja zote, Ambaye Hakuzaa na wala Hakuzaliwa, Na wala haiwi Awe na yeyote anayefanana na kulingana Naye)
Akasema: ((Naapa kwa Ambaye nafsi yangu imo Mikononi Mwake, amemuomba Allaah kwa Jina Lake Adhimu kabisa Ambalo Anapoombwa kwalo [du’aa] Anaitikia na Anapotakwa kwalo [jambo] Hutoa)) [Swahiyh Ibn Maajah (3125) Swahiyh At-Tirmidhy (3475), Swahiyh Abi Daawuwd (1493), Swahiyh At-Targhiyb (1640)]