08-Kitaab At-Tawhiyd: Tabano Au Azima Na Talasimu
Mlango Wa 8
بَابُ مَا جَاءَ فِي الرُّقَى وَالتَّمَائِمِ
Tabano Au Azima Na Talasimu[1]
فِي الصَّحِيحِ عَنْ أَبِي بَشِيرٍ الأَنْصَارِيِّ (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) أَنَّهُ كَانَ مَعَ رَسُولِ اللهِ (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) فِي بَعْضِ أَسْفَارِهِ، فَأَرْسَلَ رَسُولاً أَنْ ((لاَ يَبْقَيَنَّ فِي رَقَبَةِ بَعِيرٍ قِلادَةٌ مِنْ وَتَرٍ أَوْ قِلادَةٌ إِلاَّ قُطِعَتْ)).
Katika Swahiyh, Imepokelewa jutoka kwa Abuu Bashiyr Al-Answaariyy (رضي الله عنه) kwamba alikuwa pamoja na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) katika safari mojawapo. Akamtuma mjumbe kuamrisha kwamba: ((Kusiachwe kidani cha uzi au kidani chochote katika shingo za ngamia isipokuwa kikatwe)) [Al-Bukhaariy na Muslim]
وَعَنْ ابْنِ مَسْعُودٍ (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللهِ (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) يَقُولُ: ((إِنَّ الرُّقَى وَالتَّمَائِمَ وَالتِّوَلَةَ شِرْكٌ)) رَوَاهُ أَحْمَدُ وَأَبُو دَاودَ.
Na Imepokelewa toka kwa Ibn Mas’uwd(رضي الله عنه) kwamba Nimemsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: ((Hakika Ar-Ruqaa, At-Tamaaim na At-Tiwalah zote ni shirki)) [Ahmad, Abuu Daawuwd]
التَّمَائِمُ: شَيْءٌ يُعَلَّقُ عَلَى الأَوْلاَدِ يَتَّقَونَ بِهِ الْعَيْنَ لَكِنْ إِذَا كَانَ الْمُعَلَّقُ مِنَ الْقُرْآنِ؛ فَرَخَّصَ فِيهِ بَعْضُ السَّلَفِ، وَبَعْضُهُمْ لَمْ يُرَخِّصْ فِيهِ، وَيَجْعَلُهُ مِنَ الْمَنْهِيِّ عَنْهُ، مِنْهُمْ ابْنُ مَسْعُودٍ (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ)
والرُّقَى: هِيَ الَّتِي تُسَمَّى الْعَزَائِمَ، وَخَصَّ مِنْهَا الدَّلِيلُ مَا خَلاَ مِنَ الشِّرْكِ؛ فَقَدْ رَخَّصَ فِيهِ رَسُولُ اللهِ (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) مِنَ الْعَيْنِ وَالْحُمَةِ
والتِّوَلَةُ: هِيَ شَيْءٌ يَصْنَعُونَهُ يَزْعُمُونَ أَنَّهُ يُحَبِّبُ الْمَرْأَةَ إِلَى زَوْجِهَا وَالرَّجُلَ إِلَى امْرَأَتِهِ
At-Tamaaim: Wanachofungwa watoto (kama kitambaa cheusi au nyuzi n.k.) shingoni (au mkononi) kukinga jicho baya. Baadhi ya Salaf Swaalih wameruhusu Ikiwa imetiwa Aayah za Qur-aan, au Majina ya Allaah na Sifa Zake, lakini wengine wamekataza. Na Ibn Mas’uwd ni miongoni mwa waliokataza.
Ar-Ruqaa au Al-‘Azaaim: Ni tabano au azima inayosomwa. Imeruhusiwa tu inapokuwa haina shirki. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ameiruhusu inapokuwa hali ya kudonelewa na mdudu sumu au anapopatwa mtu na jicho baya (au hasad) au homa.
At-Tiwalah (mvuto wa ndere): Kinachodaiwa kuwa kinasababisha mwanamke apendwe zaidi na mumeme au mume apendwe zaidi na mkewe.
وَعَنْ عَبْدِ اللهِ بْنِ هُكَيْمٍ مَرْفُوعًا: ((مَنْ تَعَلَّقَ شَيْئًا؛ وُكِّلَ إِلَيْهِ)) رَوَاهُ أَحْمَدُ وَالتِّرْمِذِيُّ
Na Hadiyth Marfuw’ Imepokelewa kutoka kwa ‘Abdullaah bin Hukaym: ((Atakayetundika kitu[2] basi amejiweka katika ulinzi wa hicho kitu alichokivaa)) [na kitamdhalilisha] [Ahmad na At-Tirmidhiy]
وَرَوَى أَحْمَدُ عَنْ رُوَيْفِعٍ قَالَ؛ قَالَ لِي رَسُولُ اللهِ (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ): ((يَا رُوَيْفِعُ، لَعَلَّ الْحَيَاةَ سَتَطُولُ بِكَ؛ فَأَخْبِرِ النَّاسَ أَنَّ مَنْ عَقَدَ لِحْيَتَهُ، أَوْ تَقَلَّدَ وَتَرًا، أَوِ اسْتَنْجَى بِرَجِيعِ دَابَّةٍ أَوْ عَظْمٍ؛ فَإِنَّ مُحَمَّدًا بَرِيءٌ مِنْهُ))
Na Ahmad amepokea kutoka kwa Ruwayfi’ ambaye amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ameniambia: ((Ee Ruwayfi’! Huenda ukaishi zaidi baada yangu. Kwa hiyo wajulishe watu kwamba: Yeyote atakayefunga fundo ndevu zake, au akaweka nyuzi au mshipi shingoni mwake [kuwa ni talasimu] au akastanji na mkojo wa mnyama au mfupa, basi Muhammad amejitenga naye)) [Ahmad, Abuu Daawuwd]
وَعَنْ سَعِيدِ بْنِ جُبَيْرٍ؛ قَالَ: مَنْ قَطَعَ تَمِيمَةً مِنْ إِنْسَانٍ؛ كَانَ كَعَدْلِ رَقَبَةٍ. رَوَاهُ وَكِيعٌ وَلَهُ عَنْ إِبْرَاهِيمَ؛ قَالَ: كَانُوا يَكْرَهُونَ التَّمَائِمَ كُلَّهَا مِنَ الْقُرْآنِ وَغَيْرِ الْقُرْآن .
Kutoka kwa Sa’iyd bin Jubayr amesema: “Atakayekata talasimu au hirizi iliyovaliwa na mtu, atapata thawabu kama kuacha huru mtumwa.” Ameirekodi Wakiy’ naye pia amepokea toka kwa Ibraahiym ambaye amesema: “Walikuwa wakichukia talasimu zote ziwe za Qur-aan na zisizokuwa za Qur-aan” (walikuwa hao ni sahibu wa Ibn Mas’uwd (رضي الله عنه) .
Masuala Muhimu Yaliyomo:
1-Ufafanuzi kuhusu Ar-Ruqaa na At-Tamaaim.
2-Ufafanuzi wa At-Tiwalah.
3-Vitu vitatu vyote hivyo ni shirki na hakuna kinyume chake.
4-Ruqyah (Aayah kutoka katika Qur-aan au Adhkaar katika Sunnah) kwa ajili ya kukinga au kuondosha jicho baya au kudonelewa na mdudu sumu si shirki.
5-‘Ulamaa wametofautiana kuhusu kutumia hirizi zilokuwa na Aayah za Qur-aan.
6-Kuwavalisha mshipi (wa aina yoyote) wanyama kwa ajili ya kukinga jicho baya inapeleka katika shirki.
7-Onyo la adhabu kali kwa anayevaa vitu kama hvyo au kufunga fundo au mshipi wa aina yoyote kwa itikadi kuwa ni kinga au kuondosha madhara.
8-Thawabu za anayeikata talasimu aliyoivaa mtu.
9-Kauli ya Ibraahiym An-Nakha’iyy kuwa As-Salaf walikuwa wakijiepusha na talasimu hata ikiwa Aayah za Qur-aan au chochote, haipingani na tofauti za rai zilotajwa, kwani maneno hayo yanaashiria msimamo wa ‘Abdullaah bin Mas’uwd.