29-Kitaab At-Tawhiyd: Unajimu – Utabiri Wa nyota

Mlango Wa 29

بَابُ مَا جَاءَ فِي التَّنْجِيمِ

Unajimu – Utabiri Wa nyota

 

 

قَالَ الْبُخَارِيُّ فِي صَحِيحِهِ: قَالَ قَتَادَةُ: خَلَقَ اللَّهُ هَذِهِ النُّجُومَ لِثَلاثٍ: زِينَةً لِلسَّمَاءِ، وَرُجُومًا لِلشَّيَاطِينِ، وَعَلامَاتٍ يُهْتَدَى بِهَا، فَمَنْ تَأَوَّلَ فِيهَا غَيْرَ ذَلِكَ أَخْطَأَ وَأَضَاعَ نَصِيبَهُ وَتَكَلَّفَ مَا لاَ عِلْمَ لَهُ بِه . انْتَهَى

Al-Bukhaariy amekusanya katika Swahiyh yake: Qataadah amesema: “Allaah Ameumba hizi nyota kwa malengo matatu; (i) mapambo ya mbingu (ii) vimondo vya [kuwafukuza na kuwapiga] shaytwaan, (iii) alama za kuongoza njia (wasafiri wa majangwani na baharini). Basi atakayefasiri vingine amekosea na atakuta patupu Aakhirah (atakosa thawabu) kwani atakuwa amebeba asio na elimu nayo kwa kuchupa mipaka ya ujuzi wake.” Mwisho wa kunukuu.

 

 وَكَرِهَ قَتَادَةُ تَعَلُّمَ مَنَازِلِ الْقَمَرِ وَلَمْ يُرَخِّصِ ابْنُ عُيَيْنَةَ فِيهِ ذَكَرَهُ حَرْبٌ عَنْهُمَا وَرَخَّصَ فِي تَعَلُّمِ الْمَنَازِلِ أَحْمَدُ وَإِسْحَاقُ

Harb ameripoti kwamba kujifunza manaazil (vituo) vya mwezi imeruhusiwa na Ahmad na Is-haaq lakini imechukizwa na Qataadah na imeharamishwa na ‘Uyaynah.

 

وَعَنْ أَبِي مُوسَى قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ): ((ثَلاثَةٌ لا يَدْخُلُونَ الْجَنَّةَ: مُدْمِنُ الْخَمْرِ، وَقَاطِعُ الرَّحِمِ، وَمُصَدِّقٌ بِالسِّحْر)) رَوَاهُ أَحْمَدُ وَابْنُ حِبَّانَ فِي "صَحِيحِهِ

Imepokelewa kutoka kwa Abu Muwsaa amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Watu watatu hawatoingia Jannah; mlevi anayedumu katika pombe, mkataji undugu na anayeamini uchawi)) [Ahmad na Ibn Hibbaan katika Swahiyh yake]

 

 

Masuala Muhimu Yaliyomo:

 

1-Hikmah ya kuumbwa nyota.

 

2-Kuwakanusha wanajimu (watabiri nyota).

 

3-Khitilafu za Wanachuoni juu ya kujifunza manaazil ya mwezi.

 

4-Adhabu waliyoandaliwa wenye kuamini madanganyo ya kichawi ilhali inajulikana wazi kuwa uchawi ni upotofu.

 

 

Share