42- Kitaab At-Tawhiyd: Msimfanyie Allaah Wanaolingana Naye
Mlango Wa 42
باب: فَلَا تَجْعَلُوا لِلَّـهِ أَندَادًا وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ
Msimfanyie Allaah Wanaolingana Naye
قول الله تعالى:
Kauli ya Allaah Ta’aalaa:
فَلَا تَجْعَلُوا لِلَّـهِ أَندَادًا وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ ﴿٢٢﴾
((Basi msimfanyie Allaah waliolingana naye na hali ya kuwa nyinyi mnajua)) [Al-Baqarah (2: 22)]
وَقَالَ اِبْنُ عَبَّاسٍ فِي الآيَةِ: الأَنْدَادُ هُوَ: الشِّرْكُ أَخْفَى مِنْ دَبِيبِ النَّمْلِ عَلَى صَفَاةٍ سَوْدَاءَ فِي ظُلْمَةِ اللَّيْلِ وَهُوَ أَنْ تَقُولَ: وَاللَّهِ وَحَيَاتِكَ يَا فُلانُ، وَحَيَاتِي، وَتَقُولَ: لَوْلاَ كُلَيْبَةُ هَذَا لأَتَانَا اللُّصُوصُ، وَلَوْلاَ الْبَطُّ فِي الدَّارِ لأَتَى اللُّصُوصُ، وَقَوْلُ الرَّجُلِ لِصَاحِبِهِ: مَا شَاءَ اللَّهُ وَشِئْتَ، وَقَوْل الرَّجُلِ لَوْلاَ اللَّهُ وَفُلانٌ، لاَ تَجْعَلْ فِيهَا فُلانًا هَذَا كُلُّهُ بِهِ شِرْكٌ. رَوَاهُ اِبْنُ أَبِي حَاتِمٍ
Na Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) amesema kuhusu Aayah hiyo: ‘Andaada’ ni shirki. Nayo imefichika zaidi kama sisimizi (mweusi) apitaye juu ya jiwe jeusi katika kiza cha usiku. Mtu huingia katika shirki kama hiyo hata kwa kusema kwa utani: “Wa-Allaahi naapa kwa uhai wako na wangu ee fulani.” Pia kusema: “Lau kama si kijibwa hiki wezi wangetuingilia.” Au: “Lau sikuweko bata nyumbani wezi wangetuingilia.” Na kauli asemayo mtu kwa sahibu yake: “Maa-Shaa-Allaah wa-shiita – Kwa kupenda Allaah na wewe.” Na kauli ya mtu: “Lau kama si Allaah na fulani.” Usitaje hivyo kwani yote hii ni shirki! [Ibn Abiy Haatim]
وَعَنْ عُمَرَ بْنِ الْخَطَّابِ (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ) أَنّ رَسُولَ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) قَال: ((مَنْ حَلَفَ بِغَيْرِ اللَّهِ فَقَدْ كَفَرَ أَوْ أَشْرَك)) رَوَاهُ التِّرْمِذِيُّ وَحَسَّنَهُ وَصَحَّحَهُ الْحَاكِمُ
Na Imepokelewa kutoka kwa ‘Umar bin Al-Khattwaab (رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Atakayeapa kwa asiye Allaah, amekufuru au amefanya shirki)) [At-Tirmidhiy na ameikiri ni Hasan, na Al-Haakim ameikiri ni Swahiyh]
وَقَالَ اِبْنُ مَسْعُودٍ: لأَنْ أَحْلِفَ بِاللَّهِ كَاذِبًا أَحَبُّ إِلَيَّ مِنْ أَنْ أَحْلِفَ بِغَيْرِهِ صَادِقًا.
Ibn Mas’uwd (رضي الله عنه) amesema: “Afadhali niapie kwa Allaah jambo la uongo, kuliko kuapia asiyekuwa Allaah (au kitu kingine) hali ya kusema ukweli.”
وَعَنْ حُذَيْفَةَ (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ) أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) قَالَ: ((لاَ تَقُولُوا مَا شَاءَ اللَّهُ وَشَاءَ فُلانٌ وَلَكِنْ قُولُوا مَا شَاءَ اللَّهُ ثُمَّ شَاءَ فُلانٌ )) رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ بِسَنَدٍ صَحِيحٍ
Na Imepokelewa kutoka Kwa Hudhayfah (رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Msiseme: “Kwa kupenda Allaah na kupenda fulani” bali semeni: “Kwa kupenda Allaah kisha kupenda fulani”)) [Abuu Daawuwd kwa isnaad Swahiyh]
وَجَاءَ عَنْ إِبْرَاهِيمَ النَّخَعِيِّ: أَنَّهُ يُكْرَهُ أَعُوذُ بِاللَّهِ وَبِكَ، وَيَجُوزُ أَنْ يَقُولَ بِاللَّهِ ثُمَّ بِكَ. قَالَ: وَيَقُولُ لَوْلاَ اللَّهُ ثُمَّ فُلاَنٌ، وَلا تَقُولُوا لَوْلا اللَّهُ وَفُلانٌ.
Ibraahim An-Nakha‘iyyi alikuwa akichukia mtu kusema: “Najikinga kwa Allaah na kwako.” Lakini inafaa kusema: “Najikinga kwa Allaah kisha kwako.” Inajuzu kusema: “Lau kama si Allaah kisha fulani,” lakini haijuzu kusema: “Lau kama si Allaah na fulani.”
Masuala Muhimu Yaliyomo:
1-Maelezo ya ‘Andaad’ kama ilivyotajwa katika Aayah kwenye Suwrah Al-Baqarah (2: 22).
2-Maswahaba (رضي الله عنهم) walisema kuwa Aayah zenye kutaja shirki kubwa zilijumuisha pia na shirki ndogo.
3-Kuapa kwa asiyekuwa Allaah (سبحانه وتعالى) ni shirki.
4-Kuapa kwa asiyekuwa Allaah (سبحانه وتعالى) katika kusema ukweli ni dhambi zaidi kuliko kuapia kwa Allaah (سبحانه وتعالى) katika kusema uongo.
5-Tofauti baina ya herufi za ‘wa’ (na) na ‘thumma’ (kisha).