48-Kitaab At-Tawhiyd: Anayefanya Istihzai Chochote Kuhusu Dhikru-Allaah, Qur-aan Au Rasuli

Mlango Wa 48

بَابٌ مَنْ هَزَلَ بِشَيْءٍ فِيهِ ذِكْرُ اللَّهِ أَوْ الْقُرْآنِ أَوْ الرَّسُولِ

Anayefanya Istihzai Chochote Ndani Yake Kuna

Dhikru-Allaah au Qur-aan Au Rasuli (Ni Kufru)


 

 

وَقَوْلُ اَللَّهِ تَعَالَى:

Na kauli ya Allaah Ta’aalaa:

 

وَلَئِن سَأَلْتَهُمْ لَيَقُولُنَّ إِنَّمَا كُنَّا نَخُوضُ وَنَلْعَبُ ۚ قُلْ أَبِاللَّـهِ وَآيَاتِهِ وَرَسُولِهِ كُنتُمْ تَسْتَهْزِئُونَ ﴿٦٥﴾

((Na ukiwauliza, bila shaka watasema: “Hakika tulikuwa tunaporoja na tunacheza.” Sema:  Je, mlikuwa mnamfanyia istihizai Allaah na Aayaat Zake na Rasuli Wake?”)) [At-Tawbah (9: 65)]

 

  وَعَنِ ابْنِ عُمَرَ وَمُحَمَّدِ بْنِ كَعْبٍ وَزَيْدِ بْنِ أَسْلَمَ وَقَتَادَةَ: دَخَلَ حَدِيثُ بَعْضِهِمْ فِي بَعْضِ أَنَّهُ:  قَالَ رَجُلٌ فِي غَزْوَةِ تَبُوكَ:  مَا رَأَيْنَا مِثْلَ قُرَّائِنَا هَؤُلاَءِ أَرْغَبَ بُطُونًا وَلا أَكْذَبَ أَلْسُنًا وَلا أَجْبَنَ عِنْدَ اللِّقَاءِ – يَعْنِي: رَسُولَ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) وَأَصْحَابَهُ الْقُرَّاءَ.  فَقَالَ لَهُ عَوْفُ بْنُ مَالِكٍ :كَذَبْتَ وَلَكِنَّكَ مُنَافِقٌ لأُخْبِرَنَّ رَسُولَ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ). فَذَهَبَ عَوْفٌ إِلَى رَسُولِ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) لِيُخْبِرَه فَوَجَدَ الْقُرْآنَ قَدْ سَبَقَهُ، فَجَاءَ ذَلِكَ الرَّجُلُ إِلَى رَسُولِ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ ) وَقَدْ اِرْتَحَلَ وَرَكِبَ نَاقَتَهُ فَقَالَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، إِنَّمَا كُنَّا نَخُوضُ وَنَتَحَدَّثُ حَدِيثَ الرَّكْبِ نَقْطَعُ بِهِ عَنَاءَ الطَّرِيق.  قَالَ اِبْنُ عُمَرَ كَأَنِّي أَنْظُرُ إِلَيْهِ مُتَعَلِّقًا بِنِسْعَةِ نَاقَةِ رَسُولِ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) وَإِنَّ الْحِجَارَةَ تَنْكُبُ رِجْلَيْهِ وَهُوَ يَقُولُ: إِنَّمَا كُنَّا نَخُوضُ وَنَلْعَبُ فَيَقُولُ لَهُ رَسُولُ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم): ((أَبِاللَّـهِ وَآيَاتِهِ وَرَسُولِهِ كُنتُمْ تَسْتَهْزِئُونَ)) ((لَا تَعْتَذِرُوا قَدْ كَفَرْتُم بَعْدَ إِيمَانِكُمْ ۚ)) مَا يَلْتَفِتُ إِلَيْهِ وَمَا يَزِيدُهُ عَلَيْهِ

Imepokelewa kutoka kwa Ibn ‘Umar, na Muhammad bin Ka’b na Zayd bin Aslam na Qataadah, wamehadithia kwamba: Katika vita vya Tabuwk, mtu mmoja alisema: “Hatujapatapo kuona watu wana uchuu wa kula, waongo zaidi, waoga zaidi vitani kama wasomaji wetu hawa,” wakimaanisha Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) na Maswahaba zake wasomi wa Qur-aan. ‘Awf bin Maalik akamjibu: “Wewe ni muongo na mnafiki! Na nitamjulisha Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) [ulivyosema].” ‘Awf akaenda kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kumjulisha akakuta Aayah za Qur-aan zimeshatangulia kuteremshwa. Na yule mnafiki akamjia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) hali ameshampanda ngamia wake (yaani ameanza safari ya kurudi). Akajitolea udhuru kusema: “Ee Rasuli wa Allaah! Hakika tulikuwa tunapiga porojo na soga ili kufupisha umbali wa safari.”  Ibn ‘Umar (رضي الله عنهما)   akasema: “Kama vile namuona sasa hivi akining’inia katika mkanda wa saruji ya ngamia wa Rasuli wa Allaah na huku ngamia akikimbia na miguu yake huyo mtu ikigongwagongwa na mawe ya ardhi, naye [mnafiki akiendelea kutoa udhuru wake] akisema: “Tulikuwa tunapiga porojo na kucheza.” Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akamwambia: ((Je, mlikuwa mnamfanyia istihizai Allaah na Aayaat Zake na Rasuli Wake?”)) ((Msitoe udhuru. Mmekwishakufuru baada ya kuamini kwenu)) [At-Tawbah (9:65-66)]

 

 

Masuala Muhimu Yaliyomo:

 

1-Ni jambo la kuogopesha kuwa yeyote anayeyafanyia mchezo mambo haya (ya kufanya istihzai, dhihaka Aayah za Allaah (سبحانه وتعالى) au Rasuli Wake صلى الله عليه وآله وسلم au Waumini) amekufuru.

 

2-Maelezo yaliyotolewa ya Aayah 9: 65, yanahusu yeyote afanyae hivyo.

 

3-Kuna tofauti baina ya An-Namiymah (kufitinisha) na nasaha ya ikhlaasw kwa ajili ya Allaah (سبحانه وتعالى) na Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم).

 

4-Tofauti baina ya msamaha Anaoupenda Allaah (سبحانه وتعالى) na ukali katika kukabiliana na maadui wa Allaah (سبحانه وتعالى).

 

5- Nyudhuru nyingine haziruhusiwi.

 

Share