51-Kitaab At-Tawhiyd: Majina Mazuri Kabisa Ni Ya Allaah Basi Muombeni Kwayo
Mlango Wa 51
باب: وَلِلَّـهِ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ فَادْعُوهُ بِهَا ۖ
Majina Mazuri Kabisa Ni Ya Allaah Basi Muombeni Kwayo
قَوْلُ اَللَّهِ تَعَالَى:
Kauli ya Allaah Ta’aalaa:
وَلِلَّـهِ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ فَادْعُوهُ بِهَا ۖ وَذَرُوا الَّذِينَ يُلْحِدُونَ فِي أَسْمَائِهِ ۚ
((Na Allaah Ana Majina Mazuri kabisa, basi muombeni kwayo. Na waacheni wale wanamili katika kukadhibisha Majina Yake)) [Al-A’raaf (7: 180)]
ذَكَرَ اِبْنُ أَبِي حَاتِمٍ عَنِ اِبْنِ عَبَّاسٍ: ((يُلْحِدُونَ فِي أَسْمَائِهِ ۚ)): يُشْرِكُونَ.
Ibn Haatim ametaja kwamba Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) amesema kuhusu: ((Wanamili katika kukadhibisha Majina Yake)) yaani: wanafanya shirki.
وَعَنْهُ: سَمُّوا اَللاَّتَ مِنَ الإِلَهِ وَالْعُزَّى مِنَ الْعَزِيزِ.
Na kasema pia: “Wamewaita Al-Laata – kutokana na ‘Ilaah’. Na Al-Uzzah kutokana na ‘Al-‘Aziyz’.
وَعَنِ الأَعْمَشِ: يُدْخِلُونَ فِيهَا مَا لَيْسَ مِنْهَا
Na Al-A’mash kasema: “Wanaingiza humo (katika Majina ya Allaah, Majina) yasiyokuwemo.”
Masuala Muhimu Yaliyomo:
1-Kuthibitisha Majina ya Allaah (سبحانه وتعالى) kama Alivyosema (Al-A’raaf 7: 180).
2-Majina yote ya Allaah (سبحانه وتعالى) ni mazuri.
3-Maamrisho ya kumuomba Allaah (سبحانه وتعالى) kwa Majina Yake Mazuri.
4-Amri ya kuepukana na majahili na wakanushaji.
5-Maelezo ya wanavyopotoa na kuharibu Majina ya Allaah (سبحانه وتعالى).
6-Adhabu imeahidiwa kwa wapotoshaji Majina ya Allaah (سبحانه وتعالى).