53-Kitaab At-Tawhiyd: Kusema: Allaahumma Nighufurie Ukitaka
Mlango Wa 53
بَابٌ قَوْلُ اَللَّهُمَّ اِغْفِرْ لِي إِنْ شِئْتَ
Kusema: Allaahumma Nighufurie Ukitaka
فِي اَلصَّحِيحِ عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ : أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ (صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ): ((لا! يَقُلْ أَحَدُكُمْ: اَللَّهُمَّ اِغْفِرْ لِي إِنْ شِئْتَ، اَللَّهُمَّ اِرْحَمْنِي إِنْ شِئْتَ، لِيَعْزِمِ الْمَسْأَلَةَ، فَإِنَّ اَللَّهَ لاَ مُكْرِهَ لَهُ))
Katika Swahiyh (Al-Bukhaariy) kutoka kwa Abuu Hurayrah(رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Asiseme mmoja wenu: Ee Allaah nighufurie Ukitaka. Ee Allaah Nirehemu Ukitaka, bali aazimie [kumuomba] kwani hakuna wa kumlazimisha Allaah kufanya jambo dhidi ya Idhini Yake)) [Al-Bukhaariy]
ولِمُسْلِمٍ : ((وَلْيُعَظِّمْ اَلرَّغْبَةَ فَإِنَّ اَللَّهَ لاَ يَتَعَاظَمُهُ شَيْءٌ أَعْطَاه))
Na katika Muslim: ((Bali akuze shauku yake kwani Allaah Halioni kubwa mno jambo Alilolitoa)) [Muslim]
Masuala Muhimu Yaliyomo:
1-Kukatazwa kufanya istithnaa (kuweka masharti) katika du’aa.
2-Maelezo na sababu ya ubaya wa kusema ‘Ukitaka'.
3-Kauli ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kwamba aombe kwa azma na raghba,
4-Omba chochote upendacho kwa Allaah (سبحانه وتعالى).
5-Sababu yake (kwani hakuna limshindalo).