022-Aayah Na Mafunzo: Kumfanyia Allaah anayelingana Naye ni shirki kubwa
Aayah Na Mafunzo
Al-Baqarah
Kumfanyia Allaah anayelingana Naye ni shirki kubwa
الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ الْأَرْضَ فِرَاشًا وَالسَّمَاءَ بِنَاءً وَأَنزَلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَأَخْرَجَ بِهِ مِنَ الثَّمَرَاتِ رِزْقًا لَّكُمْ ۖ فَلَا تَجْعَلُوا لِلَّـهِ أَندَادًا وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ ﴿٢٢﴾
22. Ambaye Amewafanyieni ardhi kuwa ni tandiko na mbingu kuwa ni paa, na Akateremsha kutoka mbinguni maji, Akawatolea kwayo matunda kuwa ni riziki zenu. Basi msimfanyie Allaah waliolingana naye na hali ya kuwa nyinyi mnajua.
Mafunzo:
عَنْ عَبْدِ اللَّهِ ـ رضى الله عنه ـ قَالَ سَأَلْتُ ـ أَوْ سُئِلَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم ـ أَىُّ الذَّنْبِ عِنْدَ اللَّهِ أَكْبَرُ قَالَ: ((أَنْ تَجْعَلَ لِلَّهِ نِدًّا وَهْوَ خَلَقَكَ)). قُلْتُ ثُمَّ أَىٌّ قَالَ: ((ثُمَّ أَنْ تَقْتُلَ وَلَدَكَ خَشْيَةَ أَنْ يَطْعَمَ مَعَكَ)) قُلْتُ ثُمَّ أَىٌّ قَالَ: ((أَنْ تُزَانِيَ بِحَلِيلَةِ جَارِكَ)) قَالَ: وَنَزَلَتْ هَذِهِ الآيَةُ تَصْدِيقًا لِقَوْلِ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم ((وَالَّذِينَ لاَ يَدْعُونَ مَعَ اللَّهِ إِلَهًا آخَرَ وَلاَ يَقْتُلُونَ النَّفْسَ الَّتِي حَرَّمَ اللَّهُ إِلاَّ بِالْحَقِّ وَلَا يَزْنُونَ))
‘Abdullaah bin Mas’uwd (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amehadithia kwamba nilimuuliza au aliulizwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) Dhambi gani kubwa mbele ya Allaah? Akasema: “Kumfanyia Allaah mlinganishi (kumshirikisha) na hali Yeye Amekuumba.” Nikasema: Kisha ipi? Akasema: “Kumuua mtoto wako kwa khofu ya kutoweza kumpatia chakula chake.” Nikasema kisha ipi? Akasema: “Kuzini na mke wa jirani yako. Akasema kisha ikateremka Aayah hii kusadikisha kauli ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) : “Na wale ambao hawaombi pamoja na Allaah mwabudiwa mwengine na wala hawaui nafsi ambayo Allaah Ameiharamisha (kuuliwa) isipokuwa kwa haki, na wala hawazini.” [Al-Furqaan (25: 68) - Al-Bukhaariy na Muslim]