025-Aayah Na Mafunzo: Miongoni Mwa Neema Za Jannah

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

Miongoni Mwa Neema Za Jannah

 

 

وَبَشِّرِ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ أَنَّ لَهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ ۖ كُلَّمَا رُزِقُوا مِنْهَا مِن ثَمَرَةٍ رِّزْقًا ۙ قَالُوا هَـٰذَا الَّذِي رُزِقْنَا مِن قَبْلُ ۖ وَأُتُوا بِهِ مُتَشَابِهًا ۖ وَلَهُمْ فِيهَا أَزْوَاجٌ مُّطَهَّرَةٌ ۖ وَهُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿٢٥﴾

25. Na wabashirie wale walioamini na wakatenda mema kwamba watapata Jannaat zipitazo chini yake mito, kila watakaporuzukiwa humo katika matunda kuwa ni riziki husema: “Haya ndiyo yale tuliyoruzukiwa kabla.” Na wataletewa hali ya kuwa yanashabihiana, na watapata humo wake waliotwaharishwa, nao humo ni wenye kudumu.

 

Mafunzo:

 

 قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : ((إن أول زمرة يدخلون الجنة على صورة القمر ليلة البدر ، ثم الذين يلونهم على أشد كوكب دري في السماء إضاءة ، لا يبولون  ولا يتغوطون ، ولا يتفلون ولا يمتخطون ، أمشاطهم الذهب ، ورشحهم المسك ، ومجامرهم الألوة  الألنجوج ، عود الطيب  وأزواجهم الحور العين ، على خلق رجل واحد ، على صورة أبيهم آدم ، ستون ذراعا في السماء(( البخاري

Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Kundi la mwanzo watakaongia Jannah watakuwa kama mwezi unapokuwa kamili. Kisha watafuatia ambao watakuwa kama nyota zinazong’ara mbinguni. Hawatakojoa, wala hawatofanya haja kubwa, wala  hawatotema mate, wala hawatopenga kamasi,  vitana vyao vya dhahabu na jasho lao litanukia kama  misk,  vyetezo vyao watatumia udi wa mawardi, wake zao watakuwa ni  Huwrul-‘Ayn wenye macho mazuri makubwa. Watu watakuwa katika umbo la aina ya mtu mmoja, la baba yao Aadam wakiwa dhiraa sitini kwa urefu)) [Al-Bukhaariy]   

 

Mito yake:

 

عَنْ حَكِيم بْن مُعَاوِيَة عَنْ أَبِيهِ قَالَ سَمِعْت رَسُول اللَّه صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُول: (( فِي الْجَنَّة بَحْر اللَّبَن وَبَحْر الْمَاء وَبَحْر الْعَسَل وَبَحْر الْخَمْر ثُمَّ تَشَقَّقُ الْأَنْهَار مِنْهَا بَعْد)) وَرَوَاهُ التِّرْمِذِيّ

Imetoka kwa Hakiym bin Mu'aawiyah kutoka kwa baba yake ambaye amesema: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Katika Jannah, kuna bahari ya maziwa, na bahari ya maji, na bahari ya asali na bahari ya mvinyo [wenye ladha]) kisha mito itafunguka humo)) [At-Tirmidhiy]

 

 

 

 

Share