001-Du'aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Mema Ya Duniani Na Aakhirah Na Kinga Ya Adhabu Ya Moto
Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
Kuomba Mema Ya Duniani Na Aakhirah Na Kinga Ya Adhabu Ya Moto
Hii ni miongoni mwa du'aa alizokuwa akiomba sana Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).
رَبَّنَا آتِنَا فِي الدُّنْيَا حَسَنَةً وَفِي الأَخِرَةِ حَسَنَةً وَقِنَا عَذَابَ النَّارِ
Rabbaana aatinaa fid-dduniya hasanatan wafil Aakhirati hasanatan wa qinaa adhaaban-naari
Rabb wetu, tupe katika dunia mema na katika Akhera mema na Tukinge adhabu ya moto [Hadiyth ya Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu 'anhu kwamba ilikuwa miongoni mwa du'aa alizokithirisha kuziomba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Al-Bukhaariy, Muslim]
Faida: Du’aa hii ni ambayo imejumuisha maana nyingi ndani yake kwa kuwa imehusisha kuomba mema ya dunia na Aakhirah. Na Du’aa hii inapatikana pia ndani ya Qur-aan Suwratul Baqarah (2: 201]