004-Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Sayyid Al-Istighfaar: Du'aa Kubwa Kabisa Ya Kuomba Maghfirah Kuliko Zote
Du’aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
Sayyid Al-Istighfaar Du'aa Kubwa Kabisa Ya Kuomba Maghfirah Kuliko Zote
اللّهـمَّ أَنْتَ رَبِّـي لا إلهَ إلاّ أَنْتَ، خَلَقْتَنـي وَأَنا عَبْـدُك، وَأَنا عَلـى عَهْـدِكَ وَوَعْـدِكَ ما اسْتَـطَعْـت، أَعـوذُبِكَ مِنْ شَـرِّ ما صَنَـعْت، أَبـوءُ لَـكَ بِنِعْـمَتِـكَ عَلَـيَّ وَأَبـوءُ بِذَنْـبي فَاغْفـِرْ لي فَإِنَّـهُ لا يَغْـفِرُ الذُّنـوبَ إِلاّ أَنْتَ
Allaahumma Rabbiy laa ilaaha illa Anta Khalaqtaniy wa-ana ‘abduka wa-anaa ‘alaa ‘ahdika wawa’dika mastatwa’tu, a’uwdhu bika minsharri maa swana’tu, abuu laka bini’matika ‘alayya waabuu bidhambiy, faghfirliy fainnahu laa yaghfirudh dhunuwba illaa Anta
Ee Allaah, Wewe ni Rabb wangu, hapana Muabudiwa wa haki ila Wewe, umeniumba nami ni mja Wako, nami niko juu ya ahadi Yako, na agano Lako, kiasi cha uwezo wangu, najikinga Kwako dhidi ya shari ya nilichokifanya, nakiri Kwako kwa kunineemesha, na nakiri kwa madhambi yangu, basi nakuomba unighufurie kwani hakuna anayeghufuria madhambi ila Wewe [Al-Bukhaariy, Abu Daawuwd, At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Ibn Maajah, Ahmad - Sayyidul-Istighfaar - Du’aa kuu ya kuomba Maghfirah. Atakayesema jioni akafariki ataingia Jannah, atakayesema asubuhi akafariki ataingia Jannah.