120-Aayah Na Mafunzo: Tahadharisho La Kuwaiga Makafiri
Aayah Na Mafunzo
Al-Baqarah
Tahadharisho La Kuwaiga Makafiri
وَلَن تَرْضَىٰ عَنكَ الْيَهُودُ وَلَا النَّصَارَىٰ حَتَّىٰ تَتَّبِعَ مِلَّتَهُمْ ۗ قُلْ إِنَّ هُدَى اللَّـهِ هُوَ الْهُدَىٰ ۗ وَلَئِنِ اتَّبَعْتَ أَهْوَاءَهُم بَعْدَ الَّذِي جَاءَكَ مِنَ الْعِلْمِ ۙ مَا لَكَ مِنَ اللَّـهِ مِن وَلِيٍّ وَلَا نَصِيرٍ ﴿١٢٠﴾
120. Na hawatoridhika nawe Mayahudi wala Manaswara mpaka ufuate mila zao. Sema: “Hakika mwongozo wa Allaah ndio mwongozo (pekee).” Na ukifuata hawaa zao baada ya yale ambayo yaliyokujia katika elimu, basi hutopata kutoka kwa Allaah mlinzi yeyote wala mwenye kunusuru.
Mafunzo:
Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ameonya kuwafuata Mayahudi na Manaswara katika Hadiyth:
خَالِفُوا الْمُشْرِكِينَ أَحْفُوا الشَّوَارِبَ وَأَوْفُوا اللِّحَى
“Kuweni kinyume na washirikina, punguzeni masharubu na fugeni ndevu.” [Al-Bukhaariy na Muslim]
Na pia:
عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ، قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم: ((لَتَتَّبِعُنَّ سَنَنَ الَّذِينَ مِنْ قَبْلِكُمْ شِبْرًا بِشِبْرٍ وَذِرَاعًا بِذِرَاعٍ حَتَّى لَوْ دَخَلُوا فِي جُحْرِ ضَبٍّ لاَتَّبَعْتُمُوهُمْ)) قُلْنَا يَا رَسُولَ اللَّهِ آلْيَهُودَ وَالنَّصَارَى؟ قَالَ: ((فَمَنْ؟))
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Sa’iyd Alkhudriyy (رضي الله عنه) ambaye amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Mtafuata nyendo za wale waliokuja kabla yenu hatua kwa hatua mpaka itafika wakiingia katika shimo la kenge, na nyinyi mtaingia pia.” (Maswahaba) wakasema: Ee Rasuli wa Allaah, je, unamaanisha Mayahudi na Manaswara? Akasema: “Hivyo nani basi mwengine?” [Al-Bukhaariy na Muslim].
Pia amesema Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم):
مَنْ تَشَبَّهَ بِقَوْمٍ فَهُوَ مِنْهُمْ
“Anayejishabihisha na watu, basi naye ni miongoni mwao.” [Ahmad, Swahiyh Abiy Daawuwd (4031), na wengineo]