142-Aayah Na Mafunzo: Ahlul-Kitaab Wanatuhusudu Kwa Siku Ya Ijumaa Na Qiblah Chetu
Aayah Na Mafunzo
Al-Baqarah
Ahlul-Kitaab Wanatuhusudu Juu Ya Siku Ya Ijumaa Na Qiblah Chetu
سَيَقُولُ السُّفَهَاءُ مِنَ النَّاسِ مَا وَلَّاهُمْ عَن قِبْلَتِهِمُ الَّتِي كَانُوا عَلَيْهَا ۚ قُل لِّلَّـهِ الْمَشْرِقُ وَالْمَغْرِبُ ۚ يَهْدِي مَن يَشَاءُ إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ ﴿١٤٢﴾
142. Watasema wapumbavu miongoni mwa watu: “Nini kilichowageuza kutoka Qiblah chao ambacho walikuwa wakikielekea!” Sema: “Mashariki na Magharibi ni ya Allaah, Anamwongoza Amtakaye kuelekea njia iliyonyooka.”
Mafunzo:
Amehadithia ‘Aaishah (رضي الله عنها) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alizungumzia juu Ahlul-Kitaab akasema: “Hawatuhusudu juu ya kitu kama wanavyotuhusudu juu ya Siku ya Ijumaa ambayo Allaah Ametupa hidaaya na wao wakapotoshwa kutokana nayo. Na kwa Qiblah ambacho Allaah Ametuongoza kwacho na wao walipotoshwa kutokana nacho, na kwa kauli yetu ya ‘Aamiyn’ ya Imaam.” [Ahmad (6/134)].