163-Aayah Na Mafunzo: Aayah Mojawapo Yenye Jina Adhimu Kabisa La Allaah
Aayah Na Mafunzo
Al-Baqarah
Aayah Mojawapo Yenye Jina Adhimu Kabisa La Allaah
وَإِلَـٰهُكُمْ إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ ۖ لَّا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الرَّحْمَـٰنُ الرَّحِيمُ ﴿١٦٣﴾
163. Na Ilaah wenu (Allaah) ni Ilaah Mmoja, hapana Muabudiwa wa haki ila Yeye, Ar-Rahmaan, Mwenye kurehemu.
Mafunzo:
عَنْ أَسْمَاءَ بِنْتِ يَزِيدَ (رضي الله عنها) أَنَّ النَّبِيَّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) قَالَ: ((اسْمُ اللَّهِ الأَعْظَمُ فِي هَاتَيْنِ الأَيَتَيْنِ ((وَإِلَهُكُمْ إِلَهٌ وَاحِدٌ لاَ إِلَهَ إلاَّ هُوَ الرَّحْمَنُ الرَّحِيمُ)) وَفَاتِحَةِ آلِ عِمْرَانَ ((الم اللَّهُ لاَ إِلَهَ إلاَّ هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّوم))
Kutoka kwa Asmaa bint Yaziyd (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Jina Adhimu kabisa la Allaah limo katika Aayah zifuatazo: “Na Ilaah wenu (Allaah) ni Ilaah Mmoja, hapana Muabudiwa wa haki ila Yeye, Mwingi wa rahmah, Mwenye kurehemu.” (Al-Baqarah: 163) na na ufunguo (mwanzo) wa ‘Aal-‘Imraan: “Alif Laam Allaah, hapana Muabudiwa wa haki ila Yeye, Aliyehai daima, Msimamia kila kitu (Aal-‘Imraan: 1-2) [Swahiyh At-Tirmidhiy (3478), Swahiyh Ibn Majaah (3123), Swahiyh Al-Jaami’ (980), Swahiyh Abiy Daawuwd (1496) Swahiyh At-Targhiyb (1642)]