205-Aayah Na Mafunzo: Miongoni Mwa Ufisadi Katika Ardhi Shirki Na Bid’ah
Aayah Na Mafunzo
Al-Baqarah
Miongoni Mwa Ufisadi Katika Ardhi Shirki Na Bid’ah
وَإِذَا تَوَلَّىٰ سَعَىٰ فِي الْأَرْضِ لِيُفْسِدَ فِيهَا وَيُهْلِكَ الْحَرْثَ وَالنَّسْلَ ۗ وَاللَّـهُ لَا يُحِبُّ الْفَسَادَ ﴿٢٠٥﴾
205. Na anapoondoka hufanya bidii katika ardhi ili afisidi humo na aangamize mimea na vizazi. Na Allaah Hapendi ufisadi.
Mafunzo:
Shaykhul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema: “Kwa ujumla shirki na kumwomba du’aa asiyekuwa Allaah na kumwabudu ghairi Yake, au kumtii au kumfuata (mwongozi) asiyekuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ni ufisadi mkubwa kabisa katika ardhi, hakuna kutengenea watu wake isipokuwa mpaka iwe Allaah Ndiye Mwabudiwa Pekee na kuombwa du’aa Yeye na kumtii na ittibaa’ (kufuata mwongozo wa) Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) [Majmuw’ Al-Fataawa 25/15)]
Pia kuleta na kueneza bid’ah katika Dini. Amethadharisha Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):
مَنْ أَحْدَثَ فِي أَمْرِنَا هَذَا مَا لَيْسَ مِنْهُ فَهُوَ رَدٌّ
((Atakayezusha katika jambo letu hili (Dini yetu) basi litarudishwa.)) [Al-Bukhaariy na Muslim]