221-Aayah Na Mafunzo: Mwanamke Huolewa Kwa Sifa Nne…
Aayah Na Mafunzo
Al-Baqarah
Mwanamke Huolewa Kwa Sifa Nne….
وَلَا تَنكِحُوا الْمُشْرِكَاتِ حَتَّىٰ يُؤْمِنَّ ۚ وَلَأَمَةٌ مُّؤْمِنَةٌ خَيْرٌ مِّن مُّشْرِكَةٍ وَلَوْ أَعْجَبَتْكُمْ ۗ وَلَا تُنكِحُوا الْمُشْرِكِينَ حَتَّىٰ يُؤْمِنُوا ۚ وَلَعَبْدٌ مُّؤْمِنٌ خَيْرٌ مِّن مُّشْرِكٍ وَلَوْ أَعْجَبَكُمْ ۗ أُولَـٰئِكَ يَدْعُونَ إِلَى النَّارِ ۖ وَاللَّـهُ يَدْعُو إِلَى الْجَنَّةِ وَالْمَغْفِرَةِ بِإِذْنِهِ ۖ وَيُبَيِّنُ آيَاتِهِ لِلنَّاسِ لَعَلَّهُمْ يَتَذَكَّرُونَ ﴿٢٢١﴾
221. Na wala msiwaoe wanawake washirikina mpaka waamini. Na mjakazi Muumini ni bora kuliko mshirikina japo akikupendezeni. Na wala msiwaozeshe (wanawake wa Kiislamu) wanaume washirikina mpaka waamini. Na mtumwa Muumini ni bora kuliko mshirikina japo akikupendezeni. Hao wanaita katika moto na Allaah Anaita katika Al-Jannah na maghfirah kwa idhini Yake. Na Anabainisha Aayaat (na shariy’ah) Zake ili wapate kukumbuka.
Mafunzo:
Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Mwanamke huolewa kwa (sifa) nne; mali yake (utajiri), nasaba yake, na uzuri wake na Dini yake, lakini shikilia mwenye Dini utaneemeka.” [Al-Bukhaariy na Muslim]