269-Aayah Na Mafunzo: Fadhila Za Kujaaliwa Hikmah Na Du’aa Ya Kuomba Hikmah
Al-Baqarah
Fadhila Za Kujaaliwa Hikmah Na Du’aa Ya Kuomba Hikmah
يُؤْتِي الْحِكْمَةَ مَن يَشَاءُ ۚ وَمَن يُؤْتَ الْحِكْمَةَ فَقَدْ أُوتِيَ خَيْرًا كَثِيرًا ۗ وَمَا يَذَّكَّرُ إِلَّا أُولُو الْأَلْبَابِ ﴿٢٦٩﴾
269. Humpa hikmah Amtakaye. Na anayepewa hikmah basi kwa yakini huwa amepewa khayr nyingi. Na hawakumbuki (na kuwaidhika) isipokuwa wenye akili.
Mafunzo:
Ibn Mas‘uwd (رضي الله عنه) amehadithia kwamba alimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: “Hapana hasad ila katika mawili; mtu aliyeruzukiwa mali na Allaah na akaitumia kwa uadilifu, na mtu aliyepewa hikmah na Allaah na anahukmu kwayo na anawafundisha wengine.” [Ahmad (1/432) katika Tafsiyr Ibn Kathiyr]
الَّهُمَّ آتِنِي الْحِكْمَةَ الَّتِي مَنْ أُوتِيَهَا فَقَدْ أُوتِيَ خَيْرًا كَثِيرًا
Allaahumma aatinil-hikmatallaty man uwtiyahaa faqad uwtiya khayran kathiyraa
Ee Allaah, Nipe Hikma ambayo atakayepewa basi kwa yakini amepewa khayr nyingi. [Ad-Du’aa Minal-Kitaabi was Sunnah li Sa’iyd bin Wahf Al-Qahtwaaniy]