273-Aayah Na Mafunzo: Fadhila Za Anayejizuia Na Kustahi Kuombaomba

 

Al-Baqarah

 Fadhila Za Anayejizuia Na Kustahi Kuombaomba

www.alhidaaya.com

 

 

لِلْفُقَرَاءِ الَّذِينَ أُحْصِرُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ لَا يَسْتَطِيعُونَ ضَرْبًا فِي الْأَرْضِ يَحْسَبُهُمُ الْجَاهِلُ أَغْنِيَاءَ مِنَ التَّعَفُّفِ تَعْرِفُهُم بِسِيمَاهُمْ لَا يَسْأَلُونَ النَّاسَ إِلْحَافًا ۗ وَمَا تُنفِقُوا مِنْ خَيْرٍ فَإِنَّ اللَّـهَ بِهِ عَلِيمٌ ﴿٢٧٣﴾

273. (Swadaqah ni) Kwa ajili ya mafakiri waliozuilika katika njia ya Allaah hawawezi kwenda huku na kule katika ardhi (kutafuta rizki); asiyewajua huwadhania kuwa ni matajiri kutokana na staha ya kujizua kwao, unawatambua kwa alama zao, hawaombi watu kwa ung’ang’anizi. Na chochote mtoacho katika kheri basi Allaah kwacho ni Mjuzi.

Mafunzo:

 

Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Si maskini anayewazungukia watu anarudishwa na tonge moja au mawili na tende moja au tende mbili, lakini maskini ni yule ambaye hapati chenye kumtosheleza, wala hajulikani ili apewe swadaqah wala hasimami kuwaomba watu.” [Al-Bukhaariy (1479)]

 

Abuu Sa’iyd alisema: “Mama yangu alinituma kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kuomba msaada, lakini nilipofika nilikaa kitako, Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliniangalia na kuniambia: “Yeyote anayeridhika, Allaah Atamtajirisha. Yule anayejistahi Allaah Atamfanya aheshimike. Anayewaomba watu ambapo ana kiasi kidogo, atakuwa ombaomba.” [Imaam Ahmad (3/9) - Tafsiyr Ibn Kathiyr]

 

Share