020-Aayah Na Mafunzo: Asiyemuamini Nabiy Katika Ahlil-Kitaabi Ataingia Motoni

Aayah Na Mafunzo

Aal-‘Imraan

Asiyemuamini Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم) Katika Ahlil-Kitaabi Ataingia Motoni

www.alhidaaya.com

 

 Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa);

 

فَإِنْ حَاجُّوكَ فَقُلْ أَسْلَمْتُ وَجْهِيَ لِلَّـهِ وَمَنِ اتَّبَعَنِ ۗ وَقُل لِّلَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ وَالْأُمِّيِّينَ أَأَسْلَمْتُمْ ۚ فَإِنْ أَسْلَمُوا فَقَدِ اهْتَدَوا ۖ وَّإِن تَوَلَّوْا فَإِنَّمَا عَلَيْكَ الْبَلَاغُ ۗ وَاللَّـهُ بَصِيرٌ بِالْعِبَادِ ﴿٢٠﴾

20. Na wakikuhoji, basi sema: “Nimejisalimisha kwa Allaah na ambao walionifuata” Na waambie waliopewa Kitabu na wasiojua kusoma na kuandika: “Je, mmesilimu?” Wakisilimu basi wameongoka, na wakikengeuka basi hakika juu yako ni kubalighisha. Na Allaah ni Mwenye kuwaona waja.

 

Mafunzo:

 

Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Naapa kwa Ambaye nafsi yangu imo Mikononi mwake, hatosikia yeyote yule kuhusu mimi katika Ummah huu; Yahudi wala Naswara, kisha akafariki bila ya kuamini kwa yale ambayo nimetumwa nayo, isipokuwa basi atakuwa miongoni mwa watu wa motoni.” [Al-Bukhaariy].

 

Na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)  amesema pia:  “Na alikuwa Nabiy akitumwa kwa watu wake pekee lakini mimi nimetumwa kwa watu wote.”

 

 

Share