128-Aayah Na Mafunzo: Tukio La Kuumizwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Katika Vita Vya Uhud
Aayah Na Mafunzo
Aal-‘Imraan
Tukio La Kuumizwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Katika Vita Vya Uhud
Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
لَيْسَ لَكَ مِنَ الْأَمْرِ شَيْءٌ أَوْ يَتُوبَ عَلَيْهِمْ أَوْ يُعَذِّبَهُمْ فَإِنَّهُمْ ظَالِمُونَ ﴿١٢٨﴾
Si juu yako katika jambo hili; ima Apokee tawbah yao au Awaadhibu, kwani wao ni madhalimu. [Aal-'Imraan: 128]
Mafunzo:
Sababun-Nuzuwl:
Aayah hii imeteremka kama alivyohadithia Ibn ‘Umar (رضي الله عنه) kwamba: Alimsikia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alipoinua kichwa chake kutoka rukuu’ ya mwisho ya Swalaah ya Alfajiri baada ya kusema:
سَمِعَ اَللَّهُ لِمَنْ حَمِدَه رَبَّنَا لَكَ اَلْحَمْدُ
“Sami’a-Allaahu liman hamidah Rabbanaa Lakal-Hamd.
Allaah Amemsikia aliyemhimidi, Ee Rabb wetu, Himdi ni Zako Wewe
Kisha akasema:
اللَّهُمَّ الْعَنْ فُلَانًا وفُلَانًا وفُلَانًا
“Allaahumma mlaani fulani na fulani na fulani.” Ikateremka:
لَيْسَ لَكَ مِنَ الْأَمْرِ شَيْءٌ أَوْ يَتُوبَ عَلَيْهِمْ أَوْ يُعَذِّبَهُمْ فَإِنَّهُمْ ظَالِمُونَ ﴿١٢٨﴾
Jambo hili halikuhusu wewe; ima Apokee tawbah yao au Awaadhibu, kwani wao ni madhalimu. (3:128). [Al-Bukhaariy na wengineo kwa riwayaah nyenginezo]
Na Anas bin Maalik (رضي الله عنه) amehadithia kwamba: Siku ya Uhud, jino la Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) lilivunjika na akachomwa mkuki begani mwake. Damu ikawa inamchirizika usoni mwake akawa anaifuta damu huku akisema: “Vipi watu watafaulu ikiwa wamerowanisha uso wa Nabiy wao kwa damu na hali yeye anawalingaia kwa Allaah?” Hapo ikateremka Aayah hii:
لَيْسَ لَكَ مِنَ الْأَمْرِ شَيْءٌ أَوْ يَتُوبَ عَلَيْهِمْ أَوْ يُعَذِّبَهُمْ فَإِنَّهُمْ ظَالِمُونَ ﴿١٢٨﴾
Jambo hili halikuhusu wewe; ima Apokee tawbah yao au Awaadhibu, kwani wao ni madhalimu” (3: 128) [At-Tirmidhiy Hadiyth Hasan Swahiyh].