001-Aayah Na Mafunzo: Fadhila Za Swillatur-Rahm (Kuunga Undugu) Na Matahadharisho Ya Kukata Undugu
Aayah Na Mafunzo
An-Nisaa
Fadhila Za Swillatur-Rahm (Kuunga Undugu) Na Matahadharisho Ya Kukata Undugu
Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):
يَا أَيُّهَا النَّاسُ اتَّقُوا رَبَّكُمُ الَّذِي خَلَقَكُم مِّن نَّفْسٍ وَاحِدَةٍ وَخَلَقَ مِنْهَا زَوْجَهَا وَبَثَّ مِنْهُمَا رِجَالًا كَثِيرًا وَنِسَاءً ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ الَّذِي تَسَاءَلُونَ بِهِ وَالْأَرْحَامَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَلَيْكُمْ رَقِيبًا ﴿١﴾
Enyi watu! Mcheni Rabb wenu Ambaye Amekuumbeni kutokana na nafsi moja (Aadam) na Akaumba kutoka humo mke wake (Hawwaa) na Akaeneza kutoka hao wawili wanaume na wanawake wengi. Na mcheni Allaah Ambaye Kwake mnaombana (haki zenu kwa kuunga) undugu. Hakika Allaah ni Mwenye kuwachunga daima. [An-Nisaa: 1]
Mafunzo:
Swillatur-Rahm = Kuunga Undugu Na Jamaa Wenye Uhusiano Wa Damu:
Fadhila kadhaa zimetajwa katika Qur-aan na Sunnah za mwenye kuunga undugu na jamaa wenye uhusiano wa damu. Miongoni mwazo ni:
عن أنسٍ رضي الله عنه: أن رَسُول الله صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( من أحَبَّ أنْ يُبْسَطَ لَهُ في رِزْقِهِ ، ويُنْسأَ لَهُ في أثَرِهِ ، فَلْيَصِلْ رَحِمَهُ )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .
Imepokewa na Anas (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Anayependa akunjuliwe riziki yake, na arefushiwe maisha yake basi aunge kizazi chake." [Al-Bukhaariy, Muslim na Abu Daawuud]
Matahadharisho ya kukata undugu: Rejea tanbihi (2: 27) Pia miongoni mwa Hadiyth alizokataza Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kukata undugu ni zifuatazo:
عن أَبي هريرة رضي الله عنه، قَالَ : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( إنَّ اللهَ تَعَالَى خَلَقَ الخَلْقَ حَتَّى إِذَا فَرَغَ مِنْهُمْ قَامَتِ الرَّحِمُ ، فَقَالَتْ : هَذَا مُقَامُ العَائِذِ بِكَ مِنَ القَطِيعةِ ، قَالَ : نَعَمْ ، أمَا تَرْضَيْنَ أنْ أصِلَ مَنْ وَصَلَكِ ، وَأقْطَعَ مَنْ قَطَعَكِ ؟ قَالَتْ : بَلَى ، قَالَ : فَذَلِكَ لَكِ ، ثُمَّ قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( اقْرَؤُوا إنْ شِئْتمْ : ( فَهَلْ عَسَيْتُمْ إِنْ تَوَلَّيْتُمْ أَنْ تُفْسِدُوا فِي الأَرْضِ وَتُقَطِّعُوا أَرْحَامَكُمْ أُولَئِكَ الَّذِينَ لَعَنَهُمُ اللهُ فَأَصَمَّهُمْ وَأَعْمَى أَبْصَارَهُمْ ) [ محمد : 22 - 23 ] مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .
وفي رواية للبخاري : فَقَالَ الله تَعَالَى : (( مَنْ وَصَلَكِ ، وَصَلْتُهُ ، وَمَنْ قَطَعَكِ ، قَطَعْتُهُ )) .
Imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakika Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) baada ya kuumba viumbe vyote, mpaka Alipomaliza (kukamilisha), yalisimama matumbo (kizazi) na kusema: "Hii ni nafasi ya mtu anayetaka ulinzi na kinga kutoka Kwako kwa mwemye kukata (kizazi, na kihitaji ulinzi)." Akasema: "Ndio je huridhiki Kwangu kumuunga anayekuunga, na kumkata mwenye kukukata?" Kikasema: "Ndio (naridhika)." Akaambiwa: "Hilo ni lako." Kisha akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Someni mkitaka: "Basi huenda nyinyi mkigeuka ndio mfanye ufisadi katika ardhi na kukata jamaa zenu wa uhusiano wa damu? Hao ndio ambao Allaah Amewalaani; Akawafanya viziwi na Akawapofua macho yao." [Muhammad: 22-23] [Al-Bukhaariy na Muslim]
Na katika riwaayah ya Al-Bukhaariy: Akasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa): "Anayekuunga, Nitamuunga na anayekukata Nitamkata."
Pia:
عن عبد الله بن عمرو بن العاص رضي الله عنهما، عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( لَيْسَ الوَاصِلُ بِالمُكَافِىء ، وَلكِنَّ الوَاصِلَ الَّذِي إِذَا قَطَعَتْ رَحِمُهُ وَصَلَهَا )) رواه البخاري .
Na kutoka kwake Ibn 'Amr bin al-'Aasw (Radhwiyah Allaahu 'anhummaa): Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Anayeunga si yule anayetoa anapopewa, lakini anayeunga jamaa ni ambaye jamaa zake wanapomkata, yeye huwaunga." [Al-Bukhaariy, Abu Daawuud na At-Tirmidhiy]
Pia,
وعن عائشة ، قَالَتْ : قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: (( الرَّحِمُ مُعَلَّقَةٌ بِالعَرْشِ تَقُولُ : مَنْ وَصَلَنِي ، وَصَلَهُ اللهُ ، وَمَنْ قَطَعَنِي ، قَطَعَهُ اللهُ )) مُتَّفَقٌ عَلَيهِ .
Imepokewa kutoka kwa 'Aa'ishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Kizazi kimetundikwa katika 'Arshi, kinasema: "Anayeniunga, Allaah atamuunga, na anayenikata, Allaah Atamkata." [Al-Bukhaariy na Muslim]