100-Aayah Na Mafunzo: Anayehajiri Kwa Ajili Ya Allaah Akafariki Ataandikiwa Thawabu Zake

Aayah Na Mafunzo

An-Nisaa

Anayehajiri Kwa Ajili Ya Allaah Akafariki Ataandikiwa Thawabu Zake

Alhidaaya.com

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

 

وَمَن يُهَاجِرْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ يَجِدْ فِي الْأَرْضِ مُرَاغَمًا كَثِيرًا وَسَعَةً ۚ وَمَن يَخْرُجْ مِن بَيْتِهِ مُهَاجِرًا إِلَى اللَّـهِ وَرَسُولِهِ ثُمَّ يُدْرِكْهُ الْمَوْتُ فَقَدْ وَقَعَ أَجْرُهُ عَلَى اللَّـهِ ۗ وَكَانَ اللَّـهُ غَفُورًا رَّحِيمًا ﴿١٠٠﴾

Na anayehajiri katika njia ya Allaah atapata katika ardhi mahali pengi pa kukimbilia kujihifadhi na rizki. Na atakayetoka nyumbani kwake akiwa ni mwenye kuhajiri kwa ajili ya Allaah na Rasuli Wake, kisha mauti yakamfikia, basi ujira wake umehakikika kwa Allaah. Na Allaah daima ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu. [An-Nisaa: 100]

 

Mafunzo:

 

 

عن أَمِيرِ المُؤمِنِينَ أَبي حَفْصٍ عُمَرَ بنِ الخطَّابِ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ : سَمِعْتُ رَسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ:  إِنَّما الأَعْمَالُ بالنِّيَّاتِ وإنَّما لكُلِّ امْرِىءٍ ما نَوَى، فَمَنْ كانَتْ هِجْرَتُهُ إلى اللهِ ورَسُولِهِ فَهِجْرَتُهُ إلى اللهِ ورَسُولِهِ، ومَنْ كانَتْ هِجْرَتُهُ لِدُنْيا يُصِيبُها أو امْرأةٍ يَنْكِحُها فَهِجْرَتُهُ إلى ما هَاجَرَ إليه)).  

Kutoka kwa Amiri wa Waumuni, Abu Hafs 'Umar Ibn Al Khattwaab (Radhwiya Allaahu 'anhu) ambaye amesema: Nilimsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: “Hakika (kusihi kwa) ‘amali kunategemea niyyah, na kila mtu atapata kwa mujibu wa kile alichokinuia. Kwa hiyo ambaye hijrah yake ni kwa ajili ya Allaah na Rasuli Wake, basi hijrah yake ni kwa ajili ya Allaah na Rasuli Wake. Na ambaye hijrah yake ni kwa ajili ya manufaa ya kidunia au kwa ajili ya kumuoa mwanamke (fulani), basi hijrah yake ni kwa lile aliloliendea.[Amehadithia ‘Umar bin Khatwwaab (رضي الله عنه)  ameipokea Al-Bukhaariy na Muslim].

 

Pia Sababun-Nuzuwl: Ilipoteremka kauli ya Allaah:

 

إِنَّ الَّذِينَ تَوَفَّاهُمُ الْمَلَائِكَةُ ظَالِمِي أَنفُسِهِمْ قَالُوا فِيمَ كُنتُمْ ۖ قَالُوا كُنَّا مُسْتَضْعَفِينَ فِي الْأَرْضِ ۚ قَالُوا أَلَمْ تَكُنْ أَرْضُ اللَّـهِ وَاسِعَةً فَتُهَاجِرُوا فِيهَا ۚ فَأُولَـٰئِكَ مَأْوَاهُمْ جَهَنَّمُ ۖ وَسَاءَتْ مَصِيرًا ﴿٩٧﴾

Hakika wale ambao Malaika wamewafisha, hali wamejidhulumu nafsi zao; (Malaika) watawaambia: “Mlikuwa katika hali gani?” Watasema: “Tulikuwa tukikandamizwa katika ardhi.” (Malaika) Watasema: “Je, kwani ardhi ya Allaah haikuwa ya wasaa mkahajiri? Basi hao makazi yao yatakuwa ni Jahannam, na uovu ulioje mahali pa kuishia. [An-Nisaa: 97]

 

Palikuweko mtu mmoja Makkah akiitwa Dhwamrah, yeye alikuwa ni mgonjwa akaiambia familia yake: “Nitoeni Makkah kwani nahisi joto kali la maradhi.” Familia yake wakamuuliza: “Tukupeleke wapi?” Akaashiria kwa mkono wake kuwa wampeleke Madiynah. Hapo ikateremka Aayah hii:

 

 

وَمَن يُهَاجِرْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ يَجِدْ فِي الْأَرْضِ مُرَاغَمًا كَثِيرًا وَسَعَةً ۚ وَمَن يَخْرُجْ مِن بَيْتِهِ مُهَاجِرًا إِلَى اللَّـهِ وَرَسُولِهِ ثُمَّ يُدْرِكْهُ الْمَوْتُ فَقَدْ وَقَعَ أَجْرُهُ عَلَى اللَّـهِ ۗ وَكَانَ اللَّـهُ غَفُورًا رَّحِيمًا ﴿١٠٠﴾

Na anayehajiri katika njia ya Allaah atapata katika ardhi mahali pengi pa kukimbilia kujihifadhi na rizki. Na atakayetoka nyumbani kwake akiwa ni mwenye kuhajiri kwa ajili ya Allaah na Rasuli Wake, kisha mauti yakamfikia, basi ujira wake umehakikika kwa Allaah. Na Allaah daima ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu. [An-Nisaa: 100]

[Amehadithia Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) ameipokea Ibn Jariyr].

 

 

 

Share