114-Aayah Na Mafunzo: Kusuluhisha Baina Ya Watu Ina Daraja Bora Kabisa

Aayah Na Mafunzo

An-Nisaa

Kusuluhisha Baina Ya Watu Ina Daraja Bora Kabisa

Alhidaaya.com

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

 

لَّا خَيْرَ فِي كَثِيرٍ مِّن نَّجْوَاهُمْ إِلَّا مَنْ أَمَرَ بِصَدَقَةٍ أَوْ مَعْرُوفٍ أَوْ إِصْلَاحٍ بَيْنَ النَّاسِ ۚ وَمَن يَفْعَلْ ذَٰلِكَ ابْتِغَاءَ مَرْضَاتِ اللَّـهِ فَسَوْفَ نُؤْتِيهِ أَجْرًا عَظِيمًا ﴿١١٤﴾

Hakuna khayr katika minong’ono yao mingi isipokuwa anayeamrisha swadaqah, au mema, au kusuluhisha baina ya watu. Na atakayefanya hivyo kutaka radhi za Allaah, basi Tutampa ujira adhimu. [An-Nisaa: 114]

 

 

Mafunzo:

 

Fadhila za kusuluhisha waliokhasimikiana: Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Je, nikujulisheni lililo na daraja bora kuliko Swiyaam na Swalaah (Za Sunnah)  na Swadaqah? Ni kusuluhisha baina ya watu. Na ama kuharibu uhusiano baina (ya watu) ni uharibifu.” [Ahmad na Abuu Daawuwd na At-Tirmidhy katika Swahiyh Al-Jaami'].

 

Kwa faida ziyada bonyeza viungo vifuatavyo:

 

Fadhila Za Kusuluhisha Waliokhasimiana -1

Fadhila Za Kusuluhisha Waliokhasimiana -2

 

 

 

 

 

 

Share