030-Aayah Na Mafunzo: Anayeua Kwa Dhulma Atabeba Dhambi Za Mwana Wa Kwanza Wa Aadam
Aayah Na Mafunzo
Al-Maaidah
Anayeua Kwa Dhulma Atabeba Dhambi Za Mwana Wa Kwanza Wa Aadam
فَطَوَّعَتْ لَهُ نَفْسُهُ قَتْلَ أَخِيهِ فَقَتَلَهُ فَأَصْبَحَ مِنَ الْخَاسِرِينَ ﴿٣٠﴾
Basi nafsi yake ikamwezesha kwa wepesi kumuua ndugu yake, akamuua na akawa miongoni mwa waliokhasirika. [Al-Maaidah: 30]
Mafunzo:
Kutoka kwa Ibn Mas’uwd (رضي الله عنه) ya kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Hakuna nafsi yeyote inayouliwa kwa dhulma isipokuwa yule mwana-Aadam wa kwanza atapata sehemu yake ya madhambi (ya mauaji) kwani yeye ndiye wa mwanzo kuanzisha mauaji (alipomuua nduguye).” [Al-Bukhaariy na Muslim]