067-Aayah Na Mafunzo: Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Ametimiza Risalah
Aayah Na Mafunzo
Al-Maaidah
Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Ametimiza Risalah
يَا أَيُّهَا الرَّسُولُ بَلِّغْ مَا أُنزِلَ إِلَيْكَ مِن رَّبِّكَ ۖ وَإِن لَّمْ تَفْعَلْ فَمَا بَلَّغْتَ رِسَالَتَهُ ۚ وَاللَّـهُ يَعْصِمُكَ مِنَ النَّاسِ ۗ إِنَّ اللَّـهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْكَافِرِينَ ﴿٦٧﴾
Ee Rasuli! Balighisha yale yaliyoteremshwa kwako kutoka kwa Rabb wako. Na usipofanya, basi utakuwa hukubalighisha ujumbe Wake. Na Allaah Atakuhifadhi na watu. Hakika Allaah Haongoi watu makafiri. [Al-Maaidah: 67]
Mafunzo:
Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ametimiza Risala: Hakika Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) aliifikisha na kuitangaza Dini ya Allaah (سبحانه وتعالى) na akaieneza da’wah yake mpaka ikawafikia majini na watu. Na akawafundisha yote aliyoyaweka Allaah (سبحانه وتعالى) kuwa ni shariy’ah. Akausimamia uwajibu huu kwa nguvu zote, na Allaah (سبحانه وتعالى) Hakumfisha mpaka Alipoinyoosha kupitia yeye dini iliyopindishwa na Akayafungua kupitia yeye macho yenye upofu na kuzifungua nyoyo zilizokuwa zimefunikwa na ujinga.
Sababun-Nuzuwl:
Bonyeza kiungo kifuatacho:
067-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Maaidah Aayah 067: وَاللَّـهُ يَعْصِمُكَ مِنَ النَّاسِ