105-Aayah Na Mafunzo: Usipoizuia Dhulma Allaah Hukaribia Kukudhibu
Aayah Na Mafunzo
Al-Maaidah
Usipoizuia Dhulma Allaah Hukaribia Kukuadhibu
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا عَلَيْكُمْ أَنفُسَكُمْ ۖ لَا يَضُرُّكُم مَّن ضَلَّ إِذَا اهْتَدَيْتُمْ ۚ إِلَى اللَّـهِ مَرْجِعُكُمْ جَمِيعًا فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ﴿١٠٥﴾
105. Enyi walioamini! Jiangalieni nafsi zenu. Hawakudhuruni waliopotoka ikiwa mmeongoka. Kwa Allaah Pekee ni marejeo yenu nyote, kisha Atakujulisheni kwa yale mliyokuwa mkiyatenda.
Mafunzo:
Abuu Bakr Asw-Swiddiyq (رضي الله عنه) amesema: Enyi watu! Hakika nyinyi mnaisoma Aayah hii:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا عَلَيْكُمْ أَنفُسَكُمْ ۖ لَا يَضُرُّكُم مَّن ضَلَّ إِذَا اهْتَدَيْتُمْ ۚ إِلَى اللَّـهِ مَرْجِعُكُمْ جَمِيعًا فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ﴿١٠٥﴾
Enyi walioamini! Jiangalieni nafsi zenu. Hawakudhuruni waliopotoka ikiwa mmeongoka. Kwa Allaah Pekee ndio marejeo yenu nyote, kisha Atakujulisheni yale mliyokuwa mkiyatenda. [Al-Maaidah (5 :105)]
Hakika mimi nimemsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: "Watu pindi watakapomuona mfanya dhulma na wakawa hawakumzuwia na hiyo dhulma, basi wafahamu kuwa Allaah Hukaribia kuwaadhibu wote kwa adhabu itokayo Kwake.” [At-Tirmidhiy, Abuu Daawuwd, Hadiyth Swahiyh]