113-Asbaabun-Nuzuwl: Aal-'Imraan Aayah 113: لَيْسُوا سَوَاءً ۗ مِّنْ أَهْلِ الْكِتَابِ أُمَّةٌ قَائِمَةٌ يَتْلُونَ آيَاتِ اللَّـهِ
أسْبابُ النُّزُول
Asbaabun-Nuzuwl
Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Aayaat Za Qur-aan)
Imekusanywa na: Alhidaaya.com
Aal-‘Imraan 113-Hawako sawa sawa; miongoni mwa Ahlil-Kitaabi wako
لَيْسُوا سَوَاءً ۗ مِّنْ أَهْلِ الْكِتَابِ أُمَّةٌ قَائِمَةٌ يَتْلُونَ آيَاتِ اللَّـهِ آنَاءَ اللَّيْلِ وَهُمْ يَسْجُدُونَ ﴿١١٣﴾
113. Hawako sawa sawa; miongoni mwa Ahlil-Kitaabi wako watu wenye kusimama (kwa utiifu) wanasoma Aayaat za Allaah nyakati za usiku na wao wanasujudu (katika Swalaah).
Sababun-Nuzuwl:
Aayah hii imeteremka kama alivyohadithia Ibn Mas’uwd (رضي الله عنه) kwamba: (Siku moja) Rasuli (صلى الله عليه وآله وسلم) aliichelewesha Swalaah ya ‘Ishaa, kisha akatoka kuja kuiswali Masjid na akawakuta Swahaba (رضي الله عنهم) bado wanamsubiri. Akasema: “Uhakika wa mambo ulivyo ni kuwa hakuna yoyote katika Watu wa Dini hizi anayemdhukuru Allaah katika wakati huu isipokuwa nyinyi tu.” Hapo ikateremka Aayah:
لَيْسُوا سَوَاءً ۗ مِّنْ أَهْلِ الْكِتَابِ
Hawako sawa sawa. Miongoni mwa Watu wa Kitabu…
mpaka mwisho wa Aayah 115. [Hadiyth ya Ibn Mas’uwd ameipokea Al-Imaam Ahmad]