161-Asbaabun-Nuzuwl: Aal-'Imraan Aayah 161: وَمَا كَانَ لِنَبِيٍّ أَن يَغُلَّ ۚ وَمَن يَغْلُلْ يَأْتِ بِمَا غَلَّ يَوْمَ الْقِيَامَةِ
أسْبابُ النُّزُول
Asbaabun-Nuzuwl
Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Aayaat Za Qur-aan)
Imekusanywa na: Alhidaaya.com
Aal-‘Imraan 161-Na haikuwa (ni tabia) kwa Nabiy yeyote kukhini
وَمَا كَانَ لِنَبِيٍّ أَن يَغُلَّ ۚ وَمَن يَغْلُلْ يَأْتِ بِمَا غَلَّ يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۚ ثُمَّ تُوَفَّىٰ كُلُّ نَفْسٍ مَّا كَسَبَتْ وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ ﴿١٦١﴾
161. Na haikuwa (ni tabia) kwa Nabiy yeyote kukhini (ngawira). Na yeyote atakayekhini atakuja na kile alichokikhini Siku ya Qiyaamah. Kisha italipwa kamilifu kila nafsi yale iliyoyachuma nao hawatodhulumiwa.
Sababun-Nuzuwl:
Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) amehadithia kwamba: “Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alituma jeshi, na jeshi hilo likarejeshewa bendera yake (yaani halikukubaliwa jeshi hilo ‘amali yake hiyo). Kisha akalituma tena likarejeshewa. Halikukubaliwa ‘amali yake kwa sababu ya khiyaana iliyofanyika ya kutoweka kipande kikubwa cha dhahabu mfano wa kichwa cha mbuzi. Ndipo ikateremka:
وَمَا كَانَ لِنَبِيٍّ أَن يَغُلَّ ۚ
Na haikuwa (ni tabia) kwa Nabiy yeyote kukhini (ngawira).
[Mu’jamu Atw-Twabaraaniy]
Pia Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) amehadithia kwamba Aayah hii:
وَمَا كَانَ لِنَبِيٍّ أَن يَغُلَّ ۚ
Na haikuwa (ni tabia) kwa Nabiy yeyote kukhini (ngawira).
Imeteremshwa kuhusiana na mahameli jekundu lilopotea siku ya Badr, kisha baadhi ya watu wakasema ameichukua Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم). Wakazidi kuendelea kusema hivyo, basi na hapo Allaah Akateremsha:
وَمَا كَانَ لِنَبِيٍّ أَن يَغُلَّ ۚ وَمَن يَغْلُلْ يَأْتِ بِمَا غَلَّ يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۚ ثُمَّ تُوَفَّىٰ كُلُّ نَفْسٍ مَّا كَسَبَتْ وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ ﴿١٦١﴾
Na haikuwa (ni tabia) kwa Nabiy yeyote kukhini (ngawira). Na yeyote atakayekhini atakuja na kile alichokikhini Siku ya Qiyaamah. (3:161). [Ameipokea Abuu Daawuwd na At-Tirmidhiy, na akasema Hasan Ghariyb]