199-Asbaabun-Nuzuwl: Aal-'Imraan Aayah 199: وَإِنَّ مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ لَمَن يُؤْمِنُ بِاللَّـهِ وَمَا أُنزِلَ إِلَيْكُمْ وَمَا أُنزِلَ إِلَيْهِمْ
أسْبابُ النُّزُول
Asbaabun-Nuzuwl
Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Aayaat Za Qur-aan)
Imekusanywa na: Alhidaaya.com
Aal-‘Imraan 199-Na miongoni mwa Watu wa Kitabu wamo wanaomwamini Allaah
وَإِنَّ مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ لَمَن يُؤْمِنُ بِاللَّـهِ وَمَا أُنزِلَ إِلَيْكُمْ وَمَا أُنزِلَ إِلَيْهِمْ خَاشِعِينَ لِلَّـهِ لَا يَشْتَرُونَ بِآيَاتِ اللَّـهِ ثَمَنًا قَلِيلًا ۗ أُولَـٰئِكَ لَهُمْ أَجْرُهُمْ عِندَ رَبِّهِمْ ۗ إِنَّ اللَّـهَ سَرِيعُ الْحِسَابِ ﴿١٩٩﴾
Na miongoni mwa Watu wa Kitabu wamo ambao kwa hakika wanamwamini Allaah na yaliyoteremshwa kwenu, na yaliyoteremshwa kwao, wananyenyekea kwa Allaah, na hawabadilishi Aayaat za Allaah kwa thamani ndogo. Hao watapata ujira wao kwa Rabb wao. Hakika Allaah Ni Mwepesi Mno wa Kuhesabu. [Aal-‘Imraan (3:199)]
Sababun-Nuzuwl:
Aayah hii imeteremka alipofariki An-Najaashiy. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akaamrisha aswaliwe, wakatoka katika jangwa wakamswalia. [Al-Bukhaariy na Muslim] Imesemwa: Walipomswalia An-Najaashiy, baadhi ya watu walisema: “Unamswalia mtumwa wa kihabeshi?” Hapo ikateremka Aayah hii. [Imehadithiwa na Anas, Wahshiy na ‘Abdullaahi bin Az-Zubayr (رضي الله عنهم). Nayo imethibiti kwa irsaal kutoka kwa Hasan Al-Baswriy. “Watu wa Kitabu wamesema.” Kwa mkusanyiko wa njia zake hizi inapanda daraja na kufanywa kuwa ni hoja]